Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Benki ya Exim yatakiwa kuongeza matawi yake mkoani Iringa
Habari Mchanganyiko

Benki ya Exim yatakiwa kuongeza matawi yake mkoani Iringa

Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim, Jaffari Matundu (Kushoto) akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Iringa
Spread the love

 

BENKI ya Exim Tanzania imeombwa kuangalia namna kujitanua zaidi mkoani Iringa kwa kuongeza matawi kwenye wilaya mbalimbali za mkoa huo ili huduma zake ziweze kuwanufaisha wananchi wengi wa mkoa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Wito huo umetolewa mwisho mwa wiki na Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa, Ephraim Kyando katika hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa kwa lengo la kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Queen Sendiga, Kyando aliupongeza uongozi wa Benki hiyo kutokana na huduma zake bora zinazotolewa.

“Binafsi nimekuwa nikikoshwa na namna benki ya Exim inavyoweza kutoa huduma zake ikiwemo mikopo kwa wateja wake bila uwepo wa misuguano kwenye marejesho ya mikopo husika…hii tafsiri yake ni kwamba mpo makini kwenye utoaji wa huduma zenu na hicho ndio kitu kinachowasaidia kuepuka  migogoro na wateja wenu…hongereni sana,’’ alisema.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa, Ephraim Kyando akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, Ofisa  Mtendaji Mkuu wa  benki ya Exim, Jaffari Matundu alisema kupitia hafla hiyo  walilenga pia  kutoa fursa miongoni mwa wateja hao ili waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja.

“Pamoja na kushukuru kwa namna ambayo wateja wetu wamekuwa nasi hadi kufikia mafanikio ya ukuaji na ubora wa huduma zetu, hafla hii inatoa fursa kwa wateja wetu pia kufahamiana wao kwa wao na hivyo kufungua milango ya fursa baina yao,’’ alisema Matundu.

Alisema hali ya uchumi katika mkoa huo inatoa fursa kubwa ya ukuaji kwa benki hiyo na hiyo ndio sababu imejipanga  kuhudumia wateja  Wakubwa, Wadogo na wa Kati  ili kuleta ustawi kwenye sekta muhimu kwa mkoa huo ikiwemo biashara, kilimo na ufugaji .

“Takwimu zinaonyesha Mkoa wa Iringa umeendelea kujenga uchumi imara na endelevu, na hivyo ufanisi katika mfumo wa fedha ni moja ya mahitaji ya muhimu na ya msingi katika ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla. Benki ya Exim tumejipanga kuhakikisha tunafanikisha hilo pamoja ’’ alisema.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo alisema  benki hiyo imejipanga zaidi  kwa kuboresha mifumo na taratibu za  utoaji huduma ili ziendane na mahitaji halisi ya wateja na soko, kuongeza weledi na umahiri wa wafanyakazi pamoja na kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa itakayowezesha kuwafikia wateja wengi zaidi, kwa urahisi zaidi, mahali popote walipo na hivyo kuwaondolea ulazima wa kutembelea matawi ya benki hiyo pindi wanapohitaji huduma

“Tumejipanga kuhakikisha Benki inafanya vizuri  kwa kuweka kipaumbele katika uboreshaji wa namna ya kupata na kutumia huduma zetu. Tunataka upatikanaji na utumiaji wa huduma za Benki ya Exim uwe rahisi, huku tukiendelea kusizogeza huduma hizo karibu zaidi na wateja wetu,’’ alisema.

Mbunge viti maalum Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati

Akitoa shukrani kwa niaba ya wateja wengine wa benki hiyo, Atu Jonas pamoja na kuonyesha kuridhishwa na huduma za benki hiyo aliiomba benki hiyo izidi kujitanua mkoani humo ili huduma zake ziweze kuwafikia na wananchi wengine mkoani humo hususani wafanyabiashara na wakulima wanaohitaji huduma bora za kibenki.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 benki hiyo imezidi kujitanua ndani na nje ya nchi ambapo ambapo hadi sasa benki hiyo imefanikiwa kufungua matawi yake kwenye nchi za  Uganda, Ethiopia, Comoro na Djibouti.

1 Comment

 • Ndugu Ephraim Kyando,
  Naomba utuonyeshe ni nchi gani imeruhusu benki za nje kufungua matawi nchini kwao zaidi ya nchi za Afrika.
  Hii inaonyesha hatujui ni jinsi gani tunaibiwa utajiri wetu.
  Tuweke masharti, na wenzetu wanaruhusu benki zetu. Lakini nchi zenye uzoefu zimeruhusu tawi moja tu!
  Kuna Exim ngapi Uingereza? Kuna Standard Chatered ngapi India?
  Tupanue benki zetu….na si za nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!