Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya Exim yaombwa kujitanua zaidi Kanda ya Ziwa
Habari Mchanganyiko

Benki ya Exim yaombwa kujitanua zaidi Kanda ya Ziwa

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Filangali Mwila akizungumza na wateja wa benki ya Exim mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Spread the love

BENKI ya Exim Tanzania imeombwa kuangalia namna ya kujitanua zaidi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa hususani katika mkoa wa Mwanza kwa kufungua matawi zaidi sambamba na huduma za uwakala ili iweze kuwafikia wateja wengi katika ukanda  huo  wanaohitaji huduma za kifedha kutoka benki hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel katika hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Mwanza.

Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

Pia Mkuu huyo wa wilaya ameipongeza benki hiyo kwa huduma zake bora mkoani humo hivyo akauomba uongozi wa Exim kuangalia namna kujitanua zaidi mkoani humo kwa kuongeza matawi kwenye wilaya mbalimbali za mkoa huo ili huduma zake ziweze kuwanufaisha wananchi wengi wa mkoa huo.

“Katika kipindi chote cha uwepo wake hapa jijini Mwanza Benki ya Exim mmekuwa na mchango mkubwa kwa wakazi wa mkoa huu kwa kutoa huduma zinazowalenga haswa wakazi wa hapa ikiwemo mikopo ya biashara, mikopo ya watumishi na sasa mmekuja na huduma mahususi kwa ajili ya wajasirimali. Nashauri sasa muone umuhimu wa kujitanua zaidi katika mkoa huu na ukanda wote wa Ziwa ili wananchi wafikiwe na huduma hizi nzuri,’’ amesema Kanali Mwila.

Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim, Agnes Kaganda akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

Kanali Mwila amesema mchango wa benki hiyo mkoani humo haujaishia katika utoaji wa huduma za kifedha tu bali pia imekuwa mdau muhimu wa maendeleo ya mkoa kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii.

“Ni hivi karibuni tu tulipokea madawati takribani 100 kutoka benki ya Exim nab ado benki hii imeendelea  kufungua milango yake ya kushirikiana na serikali katika kufanikisha mipango mingine mingi ya kimaendeleo. Ni kutokana na sababu kama hizi ndio maana nasi tunawaunga mkono kwa kuwahamasisha wananchi kujiunga  na huduma zenu,’’ amesema.

Awali akizungumza kwenye hafla  iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo amesema benki hiyo imejipanga zaidi kwa kuboresha mifumo na taratibu za utoaji huduma ili ziendane na mahitaji halisi ya wateja na soko.

 

Maofisa waandamizi wa Benki ya Exim akiwepo Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Stanley Kafu (Kulia) wakibadilisha mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila (wa pili kushoto) pamoja na wageni wengine wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Mwanza

“Pia tumejipanga kuongeza weledi na umahiri wa wafanyakazi pamoja na kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa itakayowezesha kuwafikia wateja wengi zaidi, kwa urahisi zaidi, mahali popote walipo na hivyo kuwaondolea ulazima wa kutembelea matawi ya benki hiyo pindi wanapohitaji huduma zetu. Tunataka upatikanaji na utumiaji wa huduma za Benki ya Exim uwe rahisi, huku tukiendelea kusizogeza huduma hizo karibu zaidi na wateja wetu,’’ amesema.

Alisema hali ya uchumi katika mkoa huo inatoa fursa kubwa ya ukuaji kwa benki hiyo na hiyo ndio sababu imejipanga kuhudumia wateja Wakubwa, Wadogo na wa Kati ili kuleta ustawi kwenye sekta muhimu kwa mkoa huo ikiwemo biashara, kilimo na ufugaji.

“Takwimu zinaonyesha Mkoa wa Mwanza umeendelea kujenga uchumi imara na endelevu, na hivyo ufanisi katika mfumo wa fedha ni moja ya mahitaji ya muhimu na ya msingi katika ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla. Benki ya Exim tumejipanga kuhakikisha tunafanikisha hilo pamoja ’’ alisema

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 benki hiyo imezidi kujitanua ndani na nje ya nchi ambapo ambapo hadi sasa benki hiyo imefanikiwa kufungua matawi yake kwenye nchi za Uganda, Ethiopia, Comoro na Djibouti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!