Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Biashara Benki ya Exim yakabidhi zawadi ya gari kwa mshindi wa kampeni ya ‘Weka Mkwanja tukutoe’
Biashara

Benki ya Exim yakabidhi zawadi ya gari kwa mshindi wa kampeni ya ‘Weka Mkwanja tukutoe’

Viongozi waandamizi wa Benki ya Exim wakiongozwa na Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim, Andrew Lyimo (wa tatu kushoto) wakibadhi nyaraka za umiliki wa gari aina ya Toyota Vanguard kwa Muwakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya Mkoani Iringa, Christina Maria Da Silva (kulia) baada ya taasisi hiyo kuibuka mshindi wa zawadi hiyo kubwa ya promosheni ya “Weka Mkwanja tukutoe.”
Spread the love

BENKI ya Exim imekabidhi gari aina ya Toyota Vanguard kwa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya mkoani Iringa iliyoibuka mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya “Weka Mkwanja tukutoe.”

Promosheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na benki hiyo kwa lengo la kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo leo tarehe 15 Februari, 2022 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim, Andrew Lyimo amesema mshindi huyo ni miongoni mwa wateja wa benki hiyo waliofanya miamala kuanzia kiasi cha Tsh 500,000 na kuendelea.

Pia aliingia moja kwa moja kwenye droo kubwa ya kujishindia gari aina ya Toyota Vanguard na hivyo kuibuka mshindi wa zawadi hiyo kubwa.

“Mbali na mshindi huyu wa zawadi kubwa, washindi wengine 18 waliweza kujishindia zawadi ya fedha taslimu milioni moja kila mmoja katika droo mbalimbali zilizokuwa zikiendeshwa kwa usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha katika kipindi chote ch

Muwakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya Mkoani Iringa, Christina Maria Da Silva akikagua gari aina ya Toyota Vanguard wakati akikabidhiwa gari hiyo na Benki ya Exim ikiwa ni zawadi kwa taasisi hiyo baada kuibuka mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya “Weka Mkwanja tukutoe!” iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo.

a kampeni,’’ amesema Lyimo.

Amesema sambamba na zawadi hizo kampeni hiyo iliambatana na utoaji wa elimu kwa wateja wa benki hiyo ikilenga kuwahamasisha kujiwekea akiba na faida zake katika kufikia malengo yao kiuchumi.

 

“Kampeni hii ilikuwa ni moja ya njia ya benki ya Exim katika kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini ili kuongeza tija katika maendeleo ya taifa.’’amebainisha.

Akizungumza kuhusu mafanikio ya kampeni hiyo, Lyimo amesema, katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni hiyo benki hiyo ilivutia wateja wapya zaidi ya elfu 6 huku ikifikisha malengo yake kuongeza amana na akiba za wateja kwa asilimia 110.

Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya Mkoani Iringa

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Muwakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania), Christina Maria Da Silva ameishukuru Benki ya Exim kwa zawadi hiyo ya gari huku akibainisha siri ya ushindi ni kutumia benki hiyo kujiwekea amana.

“Tunawahamasisha na wa Tanzania wengine wafungue akaunti katika benki ya Exim kwa ajili ya kupata huduma bora za kibenki ikiwepo huduma kurahisishwa kupitia mifumo ya kidigitali ambapo unaweza fanya mihamala ya kibenki ukiwa ofisini au majumbani kwako kwa njia salama kabisa,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Stanley Kafu amempongeza mshindi huyo pamoja na washindi wengine waliopatikana kupitia kampeni hiyo huku pia akiwasihi wateja wa benki hiyo kuendelea kufurahia huduma za benki hiyo sambamba na kuchangamkia kampeni nyingine kama hizo kupitia benki hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Biashara

Black Gold kasino mgodi wa madini Meridianbet 

Spread the love  Dhahabu ni moja kati ya utajiri wenye thamani kubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!