Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Biashara Benki ya Exim yaahidi uwekezaji zaidi utunzaji mazingira
Biashara

Benki ya Exim yaahidi uwekezaji zaidi utunzaji mazingira

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Stanley Kafu akitoa salamu za benki hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) yaliyoambatana na zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki. Wanaomsikiliza meza kuu ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo (katikati) na Rais wa TRCS, David Kihenzile.
Spread the love

BENKI ya Exim Tanzania imeahidi kushirikiana zaidi na wadau mbalimbali sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kushiriki kikamilifu katika kuunga mkono jitihada za utunzaji mazingira hususani kwa upandaji wa miti. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ahadi ya benki hiyo imetolewa leo tarehe 11 Mei, 2022 na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Stanley Kafu katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani.

Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) yaliyoambatana na zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki.

Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Dodoma, Jalala Kizigo akishiriki zoezi la upandaji wa miti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo (katikati).

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Seleman Jafo, Kafu amesema kupitia Program za benki hiyo zijulikanayo kama ‘Exim Go Green Initiative’ na ‘Exim Cares’ benki hiyo imekuwa ikijihusisha na mikakati mbalimbali ya kijamii ikiwemo uchangiaji damu pamoja na utunzaji mazingira kupitia matawi yake yaliyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

“Kwa upande wa ukanda huu wa kati, jiji hili la Dodoma limebahatika kuwa chaguo la Benki ya Exim katika kuendesha Programu hii. Ni Kipindi kama hiki mnamo mwaka jana, tukiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda tuliweza kushirikiana na wadau wengine mkoani hapa katika kupanda takribani miti 10,000 katika kata ya Zuzu iliyopo hapa jijini Dodoma,’’ amesema Kafu.

Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Dodoma wakiongozwa na Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Dodoma, Jalala Kizigo (wa pili kulia) wakishiriki zoezi la upandaji wa miti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) yaliyoambatana na zoezi la upandaji wa miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mwishoni mwa wiki. Benki hiyo ilikuwa ni moja ya wadhamini wakubwa wa maadhimisho hayo.

Licha ya kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji miti, benki hiyo pia ilichangia fedha kiasi cha Sh mil 15 kwa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) ili kufanikisha zoezi hilo la upandaji miti.

Amesema taasisi ya kifedha nchini ikiwemo benki hiyo zimekuwa zikiguswa na athari za kiuchumi zinazotokana na kuzorota kwa sekta za uzalishaji ikiwemo kilimo kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na hiyo imekuwa moja ya sababu kubwa zinazosababisha taasisi hiyo kushiriki mstari wa mbele katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kutunza mazingira ikiwemo upandaji miti.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Jafo pamoja na kuipongeza benki hiyo pamoja na wadau wengine kwa kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira hapa nchini, aliwataka Watanzania kuungana kwa pamoja katika kujitolea utoaji wa huduma za jamii ikiwemo ushiriki wa uokoaji nyakati za majanga pamoja na ushiriki wa utunzaji wa mazingira kwa upandaji wa miti.

“Na hii ndio sababu nawapongeza TRCS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa jitihada hizi muhimu na za kizalendo. Ninaomba jitihada hizi ziendelee katika kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotokea,’’ amesema.

Awali akizungumza kwenye maadhimisho hayo Rais wa TRCS, David Kihenzile ameiomba serikali na wadau mbalimbali nchini kuendelea kuunga mkono jitihada za Shirika hilo kwa kuwa zinalenga kuisaidia jamii moja kwa moja katika masuala mbalimbali ikiwemo majanga na dharula.

“Ndio maana tumeguswa sana na uungwaji mkono tulioupata kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Exim kwa kuwa msaada wao umetuwezesha kufanikisha zoezi hili muhimu la upandaji miti pamoja na zoezi la uchangiaji damu…tunawashukuru sana tunaomba na wengine waige mfano huo kwa kuwa bado tunahitaji sana uungwaji mkono,’’ amesema Kihenzile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Biashara

Black Gold kasino mgodi wa madini Meridianbet 

Spread the love  Dhahabu ni moja kati ya utajiri wenye thamani kubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!