May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Benki ya Dunia yaikopesha Tanzani trilioni 2.34

Spread the love

 

BODI ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia (WB), imetoa mkopo wa masharti nafuu kwa Serikali ya Tanzania wa dola za Kimarekani bilioni 1.017, sawa na Sh. 2.34 trilioni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumapili, tarehe 6 Juni 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, katika ukumbi wa mikutano wa Hazina, jijini Dodoma.

Dk. Mwigulu amesema, bodi hiyo iliidhinisha mikopo mitatu ya masharti nafuu yenye jumla ya dola za Kimarekani milioni 875 sawa na Sh.2.0125 trilioni kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo nchini.

“Tarehe 3 Juni 2021, bodi hiyo iliidhinisha mkopo mwingine wenye thamani ya dola za Marekani milioni 142 sawa na Sh.326.6 bilioni na kufanya jumla ya mikopo yenye mashariti nafuu iliyoidhinishwa na bodi kwa serikali ya Tanzania kufikia minne ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 1.017 Sawa na Sh.2.34 trilioni,” amesema

“Miradi iliyopata idhini ya bodi ni Mradi wa Roads to Inclusion and Socio -economic Opprtunities (RISE), wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 300 na mradi wa Higher Education for Economic Transformation Project (HEET) wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 425.”

“Mradi wa Digital Tanzania Project (DTP) wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 250 na mradi wa Zanzibar Energy Sector Transformation and Access Project wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 142” amesema Dk.Mwigulu.

Mwigulu Nchemba

Ameitaja miradi mingine ni mradi wa RISE ambao utasaidia kuboresha barabara za vijijini na kutoa fursa za ajira takribani ajira 35,000 kwa wananchi waliopo katika vijiji nufaika pamoja na kujenga uwezo wa usimamizi endelevu wa barabara za vijijini kwa kuhusisha njia shirikishi za jamii.

“Mradi huu utahusisha ujenzi wa jumla ya kilometa 535 kwa kiwango cha lami katika wilaya sita za mikoa ya Iringa, Lindi, Geita na Tanga na ukarabati wa maeneo korofi ya barabara za vijijini nchi mzima” amesema Dk Mwigulu.

“Kuna mradi wa DTP utasaidi kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao wa Intaneti na kuboresha huduma za umma kwa kutumia digitali kwa kustawisha ekologia ya kidigitali nchini,kuhakikisha uunganishaji wa kidigitali kwa watanzania wote na kuboresha jukwaa la huduma za kidigitali.

“Mradi wa ZESTA (wa upatikanaji wa huduma bora na za uhakjika za umeme Zanzibar) utasaidia kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora, naza uhakika za umeme visiwani Zanzibar ikiwa ni pamoja nankujenga mitambo ya nguvu ya jua na msongo wa KV 132 wa kusafirishia umeme katika visiwa hivyo,” amesema

“Vile vile mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 150 kwa ajili ya mradi wa Boosting Inclusive Growth for Zanzibar (BIG-Z), unategemewa kuwasilishwa katika katika vikao vya bodi ya Benki hiyo tarehe 10 Juni 2021 kwa ajili ya kupata idhini.”

“Mradi huu utasaidia kuboresha miundombinu ya mijini katika miji ya Unguja na Pemba kwa kujenga na kuboresha barabara za lami, mifumo ya maji taka, mifereji ya maji ya mafuriko, maeneo ya uthibiti mjini Unguja na Pemba ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na uwekezaji na kukuza utalii katika visiwa vya Zanzibar” amesema Dk. Mwigulu.

Kuhusu deni la taifa amesema, deni la taifa, likijumuisha la sekta binafsi hadi mwisho wa Aprili 2021 ni dola za Marekani milioni 31,986.7 kati ya deni hilo deni la nje ni dola za Kimarekani milioni 24,477.6 na deni la ndani ni dola za Marekani milioni 7,509.1.

“Deni la serikali ni dola za Marekani milioni 26,416.8 sawa na Sh.60.71 bilioni ikijumuisha deni la nje ni dola za Marekani Milioni 18,907.7 na deni la ndani ni dola za Marekani milioni 7,509.1 sawa na Sh.17.25 bilioni” amesema Dk.Mwigulu.

Hata hivyo, Dk. Mwigulu amesema, deni hili ni himilivu na bado nchi ipo katika hatua nzuri ya kiuchumi.

error: Content is protected !!