January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Bil 422.8

Spread the love

TANZANIA imesaini mkopo wa Sh. 422.8 Bil kutoka Benki Kuu ya Dunia ili kuimarisha huduma ya afya nchini. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Akisaini mkopo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile amesema, mkopo huo unalenga kuimarisha huduma za awali za afya nchi inayolenga wajawazito, vichanga na watoto.

Likwelile amesema, huduma hiyo itahusisha zaidi katika usimamizi wa uratibu wa fedha kwa wagonjwa ili kuwa na mwitikio wa uwajibikaji, ufanisi na utawala.

Aidha mkopo huo utawezesha mipango iliyopangwa kuongeza uwajibikaji wa wafanyakazi wa idara ya afya, usambazaji wa uelewa kwa wafanyakazi wa huduma ya awali, hasa katika mikoa husika, kuongeza upatikanaji wa dawa muhimu kwenye vifaa vya huduma ya awali, pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wajawazito, vichanga na watoto.

Hata hivyo, ameishukuru hiyo na wafanyakazi wake kwa kuwapa mkopo huo kwa wakati muafaka.

“Napenda kuwashukuru pia waliofanya bidii na kufanikisha makubaliano haya leo,” amesema Likwelile na kuongeza;

“Serikali imedhamiria mageuzi endelevu katika sekta ya afya ili kufikia malengo yaliyowekwa chini ya sekta ya afya Mpango Mkakati IV ikiwa ni pamoja matokeo makubwa sasa (BRN).

“Zaidi, pia tunataka kuwahakikishia juu ya ahadi yetu ya kuendelea katika kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kirafiki kati ya Tanzania na Benki ya Dunia”.

Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Country Director amesema mpango huo utasaidia Tanzania katika kuimarisha huduma zake za awali za afya. Director amesema zaidi ya miaka 10 Tanzania imefanikisha kupunguza vifo vya watoto na kuzidi lengo la maendeleo ya milenia kuhusu vifo vya watoto.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Bernald Konga amesema mkopo huo utachangia kutekeleza mambo mbalimbali ya afya hivyo zitatumika vizuri katika kuhudumia wajawazito, vichanga na watoto.

Amesema kuwa, maisha ya Watanzania yataimarika zaidi kutokana na sekta ya afya kuzuia vifo vilivyokuwa vikitokea mara kwa mara.

Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Dk. Deo Mtasiwa ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano na serikali.

error: Content is protected !!