Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Benki ya Dunia kuondoa kwa serikali 112 bilioni  
Habari za SiasaTangulizi

Benki ya Dunia kuondoa kwa serikali 112 bilioni  

Dola za Marekani
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania, huenda ikakosa msaada wa dola za Kimarekani 50 milioni (zaidi ya Sh.112 bilioni), kufuatia hatua yake ya kupitisha sheria  ya Takwimu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa kutoka jijini Dar es Salaam na makao makuu ya benki hiyo yaliyoko Marekani zinasema, benki imekasirishwa na hatua ya serikali kupitisha sheria hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, benki imeeleza serikali kuwa sheria hiyo mpya, inaminya uhuru wa wananchi wa kupata taarifa na inakwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri na mikataba ya kimataifa.

Katika mkutano uliyopita wa Bunge, serikali iliwasilisha bungeni, marekebishi ya sheria Na. 3 ya mwaka 2018.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, mchakataji wa taarifa za tawimu, anapigwa marufuku kusambaza taarifa zake bila ruhusa ya serikali.

Sheria inataka kila anayetoa taarifa za takwimu kuthibitishwa na serikali, jambo ambalo linaelezwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa imekuja maalum kwa ajili ya kuwaziba midomo wananchi.

* World Bank Holding Up $50 Million for Tanzania Over Statistics Bill

Mabadiliko ya sheria ya takwimu yamefanyika mwezi mmoja baada ya taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Twaweza kutoa utafiti unapnyesha kuwa umaarufu wa Rais John Magufuli, umeporomoka kwa kasi.

Aidha, kupatikana kwa taarifa hizo, kumekuja katikati ya malumbano kati ya serikali na mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Zuberi Kabwe.

Zitto na serikali wamekuwa katika mvutano mkubwa kuhusu takwimu za ukuaji wa uchumi. Wakati serikali ikidai kuwa uchumi wake unaimarika, Zitto amekuwa akichambua takwimu hizo hizo za serikali kuonyesha kuwa uchumi unadidimia.

Benki ya Dunia imeionya serikali kuwa kunahitajika juhudi za makusudi katika kuhakikisha tofauti kati ya matajiri na maskini, inapunguzwa

Benki inasema, katika kukabiliana na hali ya kutokuwa na usawa wa kiuchumi pamoja na Takwimu za miaka 10 mfululizo kuonyesha uchumi unaimarika, bado hali ya wananchi haijakombolewa kutoka kwenye lindi kubwa la umaskini.

Taarifa zinaonesha kuwa wastani wa kiwango cha ukuaji wa uchumi (GDP Growth Rate) kwa mwaka 2015 ilikuwa asimilia 7 na kwamba maoteo (projections) ya kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2016-17 itafikia asilimia 7.2.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!