January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Benki ya Access yaburuzwa kortini

Spread the love

TAASISI ya Fedha ya Access Bank yenye anwani 95068, inatarajiwa kufikishwa mahakama ya usuluhishi Dar es Salaam kujibu tuhuma mbalimbali dhidi ya mfanyakazi wake. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Nyaraka ambazo Mwanahalisionline limefanikiwa kuziona mahakamani zinaonyesha CMA/DSM/KIN/R.638/15 ikiutaka uongozi wa benki hiyo kufika mbele ya tume ya usuluhishi ili kwenda kujitetea.

Taarifa hizi zinakuja ikiwa kuna nyaraka zingine zinazoonyesha kuwa benki hiyo imetuhumiwa kwa kuwanyanyasa wafanyakazi wake.

Imearifiwa kuwa hali ya manyanyaso na uonevu imezidi kuwa hatarishi na ya kutisha kwa wafanyakazi wa kawaida katika Benki ya Access hadi kufikia kusitishwa kwa huduma ya mikopo kwa wafanyakazi.

Hali hiyo imeelezwa kuwa imetokana na maamuzi ya ghafla yaliyotolewa na Mkurugenzi wa wa Access Bank Roland Coulon akielekeza kusitishwa huduma hiyo kwa wafanyakazi hata wale ambao maombi yao yalishakubaliwa au yapo kwenye hatua za mwisho.

Mwanahalisionline limefanikiwa kuona nyaraka zilizosambazwa kwa wafanyakazi nchi nzima ikisema sababu zilizotajwa kusitisha huduma hiyo ni pamoja na bank kudai kupata hasara na pia kuwa nje ya uwiano unaotakiwa na Benki Kuu.

Waraka huo ulielekeza kuwa huduma ya mikopo kwa wafanyakazi itarudishwa pale tu wenye hisa za kampuni hiyo watakapotoa kiasi kingine cha fedha ili kuendeshea benki.

Wafanyakazi wa benk hiyo wanaendelea kuulalamikia uongozi wa benk hiyo kwa kurudisha kwa kiasi kidogo huduma hiyo kwa maelezo kuwa huduma hii itarudi kikamilifu ifikapo February 2016.

“Tunaomba kwa kupitia waraka huu Benki ielewe nia yetu safi na ya dhati ya kuihitaji huduma hii kama benki nyingine zinavyowapatia wafanyakazi wake, ni aibu tunapata shida, tunanyanyasika na kuaibika mitaani wakati mwajiri wetu anao uwezo wa kutusaidia na hataki tukope sehemu nyingine kwa dhamana yake.”

Uongozi wa Benki hiyo ulipoulizwa kuhusu tuhuma hizi na kwamba wanapaswa kufika mahakama ya usuluhishi kesho umedai kuwa hadi sasa hawana taarifa.

error: Content is protected !!