Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki Exim yavutia wadau wa kilimo Nanenane
Habari Mchanganyiko

Benki Exim yavutia wadau wa kilimo Nanenane

Spread the love

HUDUMA zinazotolewa na Benki ya Exim Tanzania kwa wadau wa sekta ya kilimo zimeendelea kuwavutia washiriki wengi wa Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mmoja wa maofisa wa Benki ya Exim tawi la Mbeya, Hidelita Mwapinga (kushoto) akizungumza na wadau wa kilimo waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa Meneja wa Benki hiyo Tawi la Mbeya, Peter Mwamala alisema taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha inayatumia vema maonesho haya kutambulisha zake kwa wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo nchini wakiwemo wakulima, wachakataji wa bidhaa za mazao pamoja na wasambazaji.

“Tunashiriki maonesho haya tukiwa na dhamira kuu ya kuwa karibu zaidi na wakulima kwa kuhakikisha kwamba wanazifahamu huduma zetu zinazohusiana na sekta ya kilimo ikiwemo huduma za malipo pamoja na fursa za mikopo.

Tupo tayari kuwahudumia! Timu ya maofisa wa benki ya Exim tawi la Mbeya wakiongozwa na Meneja wa Benki hiyo Tawi la Mbeya, Peter Mwamala (wa tatu kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

“Zaidi pia tunayatumia maonesho haya kupata kutoa huduma zetu za kifedha kwa wateja wetu waliopo kwenye maonesho haya huku pia tukipata mrejesho wa huduma zetu kutoka kwa wateja,’’ alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!