Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Benki CRDB wapewa ushauri
Habari Mchanganyiko

Benki CRDB wapewa ushauri

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela
Spread the love

WATEJA wa benki ya CRDB mkoa wa Mwanza wameishauri benki hiyo kuboresha huduma zake za kifedha ili kuwafikia wananchi wengi walioko vijijini, wakiwemo wakulima na wafanyabiashara wadogo kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Ushauri huo umetolewa wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya kumtambulisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa wateja wake wa Mwanza. 

Katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa CRDB, Ally Hussen alitumia fursa hiyo kueleza historia fupi ya benki hiyo tangu ilipofahamika kama benki ya Usharika na Maendeleo Vijijini (CRDB) mpaka mabadiliko yake na jinsi ilivyongozwa na Dk. Charles Kimei kwa kipindi cha miaka 22 kuanzia mwaka 1998 hadi Oktoba 2018.

“Bank hii ilianzishwa ikiwa na mtaji wa Sh. milioni 54,lakini hadi Dk.Kimei anaondoka ameicha benki hii ikiwa na fedha kiasi Cha zipatazo trioni 6,wakati inaanza ilipata hasara ya shilingi milioni 2,lakini baada ya mwaka mmoja ilianza kutengeneza faida hadi sasa, alisema Hussein.

Mwenyekiti huyo wa bodi amesema benki hiyo chini ya Dk. Kimei imekuwa ni chachu ya kuongeza pato la Taifa ambapo hadi mwaka 2015, walitoa kodi kwa serikali,  bilioni 44 nje na kodi ya wafanyakazi.

Alisema benki hiyo ndio inayoongoza katika ulipaji wa kodi kubwa kuliko benki nyngine hapa nchini jambo ambalo wanaendelea kujivunia.

Husseni akimwelezea Mkurugenzi mpya  alisema mkurugenzi huyo mpya alianza kufanya kazi katika benki hiyo kisha kuondoka,hivyo amerudi tena nyumbani akiwa tofauti sana maana amekuja na uzoefu mkubwa na akiwa bado ana nguvu.

Kwa upande wake Mkurugenzi mpya bwana Nsekela amesema Mwanza ni kitovu cha uchumi wa nchi,hivyo benki hivyo inatambua umuhimu wa mkoa huo kwa wateja wake wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo.

“Nina uzoefu kwenye mambo ya benki kwa miaka 21,nilifanya kazi katika CRDB miaka 11 nikaondoka kwa miaka 10 na sasa nimerudi nyumbani, mengi niliyojifunza huko sasa nayafanyia kazi nyumbani,naahidi kuwa tutafanya kazi kwa mshikamano na kupiga hatua mara dufu ya hapa tulipo sasa,” amesema Nsekela.

Pia Nsekela amesema CRDB ina matawi yasiyopungua 265 ina mitandao isiyopungua 550 pia inatoa huduma mbalimbali, kupitia mawakala zaidi ya 5,000,huduma zote zikiwalenga wateja wa mijini na vijijini na benki hiyo imeendelea kupanua wigo wa kutoa huduma kwa jamii pamoja na kuanzisha kampuni tatu,ikiwemo inayotoa huduma ya bima kwa watanzania.

Christopher Gachuma ambaye ni mmoja wa wana hisa katika pia ni mteja katika benki ya CRDB,aliwataka wateja wa wenzake wategemee maendeleo mazuri kufuatia ujio wa mkurugenzi mpya aliyekuja maana ana uzoefu katika masuala ya benki huku akidai zaidi ya asilimia 70 ya benki hiyo zimewekezwa na watanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!