BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imezipiga faini benki tano kwa ukiukwaji wa kanuni za Sheria ya Utakatishaji Fedha Haramu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BoT tarehe 19 Septemba 2019, inaeleza kwamba benki hizo zimekiuka kauni tatu za sheria ya utakatishaji fedha haramu, ambazo ni namba 17, 22 na 28. Kwa kushindwa kuwasilisha ripoti ya wateja zake, katika Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU).
Benki zilizopigwa faini ni African Banking Corparation (T) Limited iliyotozwa faini ya Sh. 145 milioni, Equity Bank Tanzania Limited (580 milioni), I&M (T) Limited (655 milioni), UBL Bank (T) Limited (325 milioni) na Habib African Bank Limited (175 milioni.)
Taarifa hiyo ya BoT inaeleza kwamba benki hizo zinatakiwa kulipa faini husika katika kipindi cha miezi mitatu tangu tarehe waliyopigwa faini.
BoT imezitaka benki na taasisi za fedha nchini kufuata sheria na kanuni zilizowekwa katika utekelezaji w amajukumu yao.
Leave a comment