May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Beki Yanga apata pigo, afiwa na watu wawili kwa mpigo

Bakari Mwamnyeto

Spread the love

BEKI wa kati na nahodha msaidizi wa klabu ya Yanga, Bakari Mwamnyeto amepata pigo kwa kufiwa na mchumba wake pamoja na mtoto usiku wa kuamkia leo kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akijifungua. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwamnyeto moja ya wachezaji waliokuwa kambini kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambacho kinajiandaa na michuano ya Kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani ‘Chan.’

Kwa upande wa Yanga kupitia Afisa Habari na mhamasishaji wa klabu klabu hiyo, Antonio Nugaz katika kuthibitisha taarifa hizo amesema kuwa “bado taratibu za msiba zinafanyika na zitakapokamilika wataweka wazi unafanyika wapi.”

Yanga kupitia kurasa yao ya kwenye mtandao wa Instagram wametuma salamu za rambirambi kwa beki wao huyo pamoja na ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo.

Kwasasa kikosi cha Yanga kipo visiwani Zanzibar kwenye kombe la Mapinduzi ambapo leo kitashuka dimbani majira ya saa 2:15 kuwakabili Namungo FC kwenye mchezo wa kundi A, utakaopigwa kwenye uwanja wa Amani.

error: Content is protected !!