May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Beki wa zamani wa Liverpool atua Ikulu Zanzibar

Rais Dk Hussein Mwinyi (kulia) akimkabidhi zawadi Mamadou Sakho (katikati) mara baada ya kumtembelea Ikulu visiwani Zanzibar

Spread the love

Beki wa zamani wa Liverpool na klabu ya Crystal Palace kwa sasa Mamadou Sakho amekutana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Hussen Mwinyi leo Ikuru visiwani humo na kufanya mazungumzo kuhusu kukuza michezo visiwani humo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Sakho amekuja katika mapumziko nchini mara baada ya msimu wa Ligi Kuu England kumalizika akiambatana na familia yake.

Katika mazungumzo yake na mchezaji huyo Rais Mwinyialisema kuwa wamekubaliana kwa pamoja na Sakho kuanzisha kituo cha michezo cha watoto kitakacho wapa fursa vijana wengi visiwano humo.

“Nimefurahi uwepo wako na tupo tayari kushirikiana nawe kuanzisha kituo cha michezo cha watoto, tuwape vijana wetu nafasi.”alisema Dk Mwinyi

Katika hatua nyingine mchezaji huyo amekubali ombi la bodi ya utalii Tanzania (TTB) kuwa balozi wa Hiyari wa utalii wa Tanzania wakati alipokutana na Betrita Lyimo ambaye ni kaimu mkurugezni mkuu wa bodi hiyo katika hifadhi ya bonde la Ngorongoro.

Kufuatia kukubali ombi hilo tayari timu ya waandishi wa habari wa Televishen ya TF1 ya nchini Ufaransa imewalisili pia nchini Tanzania tarehe 27/5/2021 kwa lengo la kutengeneza makala maalumu ya ziara ya Mamadou itakayotumika kutangaza Utalii wa Tanzania kwenye Soko la Utalii la Ufaransa hususani maeneo yote ya vivutio vya utalii aliyotembelea.

Mchezaji huyo alifika nchini toka tarehe 26 Mei, 2021 kwa ajili ya mapumziko ya siku 10, akiwa na familia yake na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kijiji cha wamasai na seneto pamoja na visiwa vya Zanzibar.

error: Content is protected !!