May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Beki mpya Yanga kuikosa Congo dhidi ya Stars kesho

Dickson Job

Spread the love

BEKI wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Dickson Job ataukosa mchezo wa kesho wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya DR Congo mara baada ya kuumia nyama za paja akiwa mazoezini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezaji huyo ambaye hii leo ametambulishwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye dirisha dogo la usajili baada ya kocha wa Yanga, Cedric Kaze kuvutiwa na kiwango chake.

Taarifa za majeruhi yake zimekuja leo tarehe 11 Januari 2021, wakati kocha msaidizi wa Taifa Stars, Juma Mgunda akieleza hali ya kikosi na maandalizi yao katika mkutano na waandishi wa Habari.

Juma Mgunda, Kocha msaidizi wa Taifa Stars

Mgunda alisema kuwa wanaendelea na maandilizi na mchezo huo utakuwa kipimo kuelekea michuano ya kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) yatakayofanyika Cameroon tarehe 19 Januari, 2021.

“Mandalizi yetu yapo vizuri na tunaamini kuwa mchezo wa kesho ni kipimo kizuri kuelekea Cameroon kwenye CHAN ila tuna majeruhi ya mchezaji mmoja ambaye ni Dickson Job ambaye ameumia nyama za paja,” alisema Mgunda.

Mchezo huo dhidi ya DR Congo utachezwa kesho majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo tayari wapinzani wa Stars wameshawasili nchini.

Kikosi cha Taifa stars kitaondoka nchini Alfajiri ya tarehe 14, kuelekea nchini Cameroon kwenye michuano hiyo ambapo Tanzania inashiriki kwa mara ya pili.

error: Content is protected !!