May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Beki Man City atwaa tuzo ya mchezaji bora EPL

Spread the love

 

RUBEN Dias mlinzi wa kati wa klabu ya Manchester City na timu ya Taifa ya Ureno ameshinda tuzo ya mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu nchini England (Epl) kwenye msimu wa 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mlinzi huyo ametwa tuzo hiyo mara baada ya kuonekana kuwa muhimili mkubwa kwenye eneo la ulinzi la Man City mpaka kufanikisha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo.

Mchezaji huyo mpaka sasa ametwaa tuzo mbili kwenye msimu huu mara baada ya kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa waandishi wa Habari za soka Epl.

Licha ya kutwaa tuzo hizo lakini Dias bado yupo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa soka la kulipwa inayopigiwa kura na wachezaji wa EPL ( The Professional Footballers’ Association Men’s Players’ Player of the Year  )

Dias ametwaa tuzo ya mchezaji boea epl mara baada ya kuwashinda kiungo wa Manchester United Bruno Fernandes, Harry Kane mshambuliaji wa Tottenham, kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Kelvin De Bruyne, na mshambuliaji wa Aston Villa na Jack Glealish.

Wengine ni mshambuliaji wa timu ya Liverpool Mohammed Salah, Tomas Soucek kutoka Westham na Mason Maount wa klabu ya Chelsea.

 

 

 

error: Content is protected !!