Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Bei ya petroli yapaa, dizeli yashuka
Habari MchanganyikoTangulizi

Bei ya petroli yapaa, dizeli yashuka

Spread the love

 

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Julai ambapo bei ya petroli imeongezeka na ile ya dizeli ikishuka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …  (endelea). 

Bei ya nishati ya petroli imepanda kutoka Sh3,194 hadi Sh3,220 huku dizeli ikishuka hadi Sh3,143 ikilinganishwa na bei za mwezi Mei.

Bei hizo zitaanza kutumika kesho Jumatano tarehe 6 kuanzia saa 6:01 usiku.

Hata hivyo bei hizo ni pungufu ya bei halisi za mwezi Julai baada ya serikali kuweka ruzuku ya Sh100 bilioni ambapo kiasi kikubwa cha ruzuku kimeelekezwa kwenye dizeli kutokana na nishati hiyo kutumika zaidi kwenye shughuli za kiuchumi.

Bei halisi za mwezi Julai kabla ya ruzuku petroli ni Sh3,497 na dizeli ni Sh 3,510 hivyo kufanya ruzuku iliyotolewa kwa kila lita ya petroli kuwa 277 na Sh 367 kwa kila lita ya dizeli.

Bei hizo ni kwa mkoa wa Dar ea Salaam na mikoa mingine bei itapungua au kuongezeka kwa kuzingatia gharama za usafirshaji kutoka bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!