Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Bei ya petroli, dizeli yashuka Tanzania
Habari Mchanganyiko

Bei ya petroli, dizeli yashuka Tanzania

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) nchini Tanzania imesema, bei ya mafuta ya taa, petrol na dizeli zimepungua kwa baadhi ya mikoa kuanzia leo Jumatano tarehe 6 Mei 2020. Anaripoti Mwandishi wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godfrey Chibulunje amesema bei za jumla na rejareja za mafuta ya petroli, dizelina na mafuta ya taa yaliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 1 Aprili 2020.

Amesema kwa Mei 2020, bei za rejareja za petrol imepungua kwa Shilingi 219/lita (sawa na asilimia 10.50), dizeli Shilingi 143/lita (sawa na asilimia 7.17) na mafuta ya taa yakipungua kwa Shilingi 355/lita (sawa na asilimia 18.47), mtawalia.

Kwa maana hiyo, Dar es Salaam petrol inauzwa kwa Shilingi 1,868, dizeli Shilingi 1,846 na mafuta ya taa Shilingi 1,568.

Chibulunje amesema bei za jumla za petrol imepungua kwa Shilingi 218.59/lita (sawa na asilimia 11.14), dizeli kwa Shilingi 142.25/lita (sawa na asilimia 7.63) na mafuta ya taa zimepunguakwa kwa Shilingi 354.09/lita (sawa na asilimia 19.69).

Amesema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli katika mkoa wa Tanga zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 1 Aprili 2020.

Amesema Mei 2020, bei za rejareja za petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini (yaani Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara) zimepungua kwa Shilingi 463/lita(sawa na asilimia 21.88) na Shilingi 377/lita (sawa na asilimia 18.21),mtawalia.

Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za petroli na dizeli zimepungua kwa Shilingi 461.82/lita (sawa na asilimia 23.19) na Shilingi375.82/lita (sawa na asilimia 19.33).

Bosi huyo wa Ewura amesema bei za mafuta ya taa kwa mikoa ya Kaskazini zitaendelea kuwa zile zilizochapishwa katika toleo la tarehe 1 Aprili 2020 kwa sababu hakuna shehena ya bidhaa hiyo iliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Tanga kwa mwezi Aprili 2020.

Kwa mwezi Mei 2020, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya dizeli katika mikoa ya Kusini (yaani Mtwara, Lindi na Ruvuma) hazitabadilika ikilinganishwa na toleo lililopitala tarehe 1 Aprili2020 kutokana na kuwa hakuna shehena ya dizeli iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara.

Hata hivyo, bei za mafuta ya petroli zimepungua ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita.
Kwa mwezi Mei 2020, bei za jumla na rejareja za petroli zimepungua kwa Shilingi 129/lita (sawa na asilimia 5.67) na Shilingi 128.14/lita (sawa na asilimia 5.99).

Kwa kuwa hakuna Mafuta ya Taa katika bandari ya Mtwara, wamiliki wa vituo vya mafuta katika mikoa tajwa wanashauriwa kununua mafuta hayo kutoka Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa kwa mikoa hiyo zinatokana na gharama za mafuta hayo kutokea Dar es Salaam na kusafirishwa hadi mkoa husika.

“Mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la ndani yanatokana namabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji (BPS Premium),” amesema Chibulunje

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!