July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bei ya nyama Dodoma kupanda

Spread the love

WAFANYABIASHARA wa maduka ya nyama ya ng’ombe katika halmashauri ya Dodoma wametangaza kupandisha bei ya nyama kutoka Sh 6,000 hadi Sh 7,000 itakayoanza rasmi kesho. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Wafanyabiashara hao wanadai kuwa wanalazimika kupandisha bei ya nyama kutokana na kuwepo uhaba mkubwa wa wanyama.

Mmoja wa wafanyabiashara ya maduka ya nyama Ally Kalumbo amesema wanalazimika kupandisha bei ya nyama kutokana na kuwepo kwa uhaba wa nyama.

“Kwa sasa tumeweka matangazo ili kuwataarifu wateja wetu juu ya kupandishwa kwa bei ili wanapokuja kununua nyama wawe wana taarifa kamili,” amesema Kalumbo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanya biashara wa nyama ya ng’ombe, Thomasi Kuhura ameeleza kuwepo kwa hali mbaya na kupanda kwa bei ya ng’ombe.

Licha ya kutokutaja bei imepanda kwa kiasi gani kwa ng’ombe mmoja amesema hata upatikani wa ng’ombe umekuwa mgumua.

Katika kuthibitisha hilo, Meneja uzalishaji wa machinjio ya kisasa iliyopo Kizota katika manispaa ya Dodoma, Khamis Kissoi amesema kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa ng’ombe kwa sasa.

Kissoi amesema kwa sasa machinjio hiyo imekuwa ikipokea ng’ombe zaidi ya 180 lakini kwa sasa imeshuka hadi kupokea ng’ombe 150 kwa siku za jumapili.

Kwa siku za kawaida machinjio imekuwa ikipata ng’ombe wa kuchinja 100 na kushuka hadi kufikia hadi 80.

Kissoi amesema kwa sasa uchinjaji wa nyama katika machinjio hiyo umeshuka kati ya asilimia kumi hadi kumi na tano.

Wakati huohuo Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma inakusudia kujenga machinjio ya kisasa na mnada wa kisasa kwa ajili ya uchinjaji na kuuza nguruwe.

Hayo yaloelezwa na Ofisa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Dodoma, Dk. Bonphace Tibaijuka alipokuwa akizungumzia hali ya mifugo na masoko katika halmashauri hiyo.

Mbali na hilo alitakiwa kutoa ufafanuzi juu ya kuwepo kwa taarifa za kupanda kwa bei ya nyama kutoka Sh. 6000 kwa kilo na kuuzwa kwa sh.7000.

Awali wafanyabiashara wa maduka ya nyama wamelazimika kupandisha bei ya nyama kutoka Sh. 6000 kwa kilo hadi sh 7000 kwa kilo kutokana na madai kuwa kwa sasa kuna uhaba wa wanyama.

Dk. Tibaijuka amesema licha ya kutokuwepo ofisini kwa kipindi kirefu lakini hakuna tatizo lolote la ukosefu wa mifugo hadi kufikia hatua ya kupandisha nyama.

Amesema katika halmashauri ya Dodoma kuna jumla ya minada saba ambayo yote inafaa katika kutoshereza mahitaji ya wakazi wa Dodoma.

Hata hivyo Dk.Tibaijuka alisema kwa bado wafugaji hawajaweza kufaidi mifugo yao kwani wanajikuta wakiuza kwa bei ndogo kutokana na kutokuwa bei ambazo zinakubalika.

Mbali na hilo amesema kwa sasa wafugaji wanapunjwa pale wanapouza mifugo yao kwani hakuna mfumo mzuri wa uuzaji wa mifugo.

Amesema kutokana na hali hiyo kuna kila sababu ya kuthaminisha ubora, uzito wa mifugo ili kuhakikisha inapatikana bei inayotakiwa badala ya kufanya uuzaji kama ilivyo sasa.

error: Content is protected !!