August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bei ya mafuta yazidi kupaa tena

Spread the love

BEI ya mafuta imepanda tena mwezi huu na kuivuka ile ya Julai licha ya Serikali kuendelea kutoa ruzuku ya Sh bilioni 100 kwa mwezi Agosti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Julai mwaka huu bei ya rejareja jijini Dar es Salaam ilikuwa Sh 3,220 kwa lita moja ya petroli na Sh 3,143 kwa dizeli huku mafuta ya taa yakifika Sh 3,442.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa leo Jumanne Agosti 2, 2022 na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), bei ya rejareja jijini Dar es Salaam baada serikali kuweka ruzuku ya Sh bilioni 100, itakuwa Sh 3,410 kwa lita moja ya petroli na Sh 3,322 kwa dizeli huku mafuta ya taa yakifika Sh 3,765.

Katika mkoa wa Tanga itakuwa Sh 3435 kwa lita moja ya petrol na Sh 3,349 kwa lita moja ya dizeli. Mkoa wa Mtwara itakuwa Sh 3,393 kwa lita moja ya petrol ilihali dizeli itakuwa Sh 3,351.

Maumivu yatakuwa makali mkoani Kagera hasa katika Wilaya ya Kyerwa ambako lita moja ya petroli itauzwa Sh 3,647 na dizeli Sh 3,560 na mafuta ya taa ni Sh 4,003.

Ewura imesema bei hizo mpya ambazo zitaanza kutumika kesho Jumatano zimejumuisha ruzuku ya Sh bilioni 100 iliyotolewa na Serikali.

Kama ruzuku hiyo isingetolewa, lita ya petrol ingeuzwa Sh 3,630, dizeli Sh 3,734 na mafuta ya taa Sh 3,765 jijini Dar es Salaam wakati Bukoba ingekuwa Sh 3,845 kwa petroli na Sh3,950 kwa dizeli. Mafuta ya taa hayana ruzuku.

“Bei ya mafuta katika soko la dunia imeendelea kupanda na bei ya mafuta katika soko la ndani kupanda vilevile. Lakini katika kupunguza kupanda kwa bei hizo, serikali imetoa ruzuku ya Sh bilioni 100 kupunguza makali ya bei hizo,” imesema taarifa hiyo.

error: Content is protected !!