May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bei ya mafuta: Rais Samia aongoza kikao usiku Ikulu, atoa maagizo

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo la kupanda bei ya mafuta nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Ametoa maagizo hayo katika kikao cha dharura alichokiitisha usiku wa jana Jumapili tarehe 8 Mei 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam kilichokuwa na lengoa kujadili tatizo hilo.

Mafuta ya petroli na dizeli yamefikia zaidi ya Sh.3,000 kwa lita hali ambayo imesababisha baadhi ya huduma kuanza kupanda kama bei za nauli za mabasi daladala, Bajaj, bodaboda na mabasi ya mikoani.

Aidha, Rais Samia ametoa maagizo hayo ikiwa imebaki siku moja kati ya tano alizopewa Waziri wa Nishati, January Makamba na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ya kutoa majibu ya serikali ya hatua ya dharura wanayochukua ili kupunguza ukali wa maisha yanayotokana na kupanda kwa nishati hiyo.

Waziri Makamba atatoa taarifa hiyo kesho Jumanne Bungeni.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho cha Rais Samia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

error: Content is protected !!