Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Bei ya dizeli yazidi kupaa, ruzuku yawekwa kando
Habari MchanganyikoTangulizi

Bei ya dizeli yazidi kupaa, ruzuku yawekwa kando

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini huku mafuta ya dizeli yakizidi kupaa.

Bei hizo zitaanza kutumika kuanzia leo Jumatano, tarehe 4 Januari 2023 saa 6:01 usiku. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Modestus Lumato imeonyesha jiji la Dar es Salaam bei ya mafuta ya dizeli itaongezeka hadi Sh3, 295 mwezi huu ikitokea Sh 3,247 Desemba, 2022

Katika mikoa ya Tanga na Mtwara bei ya mafuta ya dizeli imeongezeka kwa Sh91 na Sh135 kwa lita mtawalia.

Aidha, amesema bei ya mafuta ya petroli imepungua kidogo hadi Sh2,819 mwezi huu kutoka Sh2,827 Desemba jijini Dar es Salaam, ilihali katika mikoa ya Tanga na Mtwara imeongezeka pakubwa kwani watauza mafuta hayo kwa Sh2,993 na Sh2,979 mtawalia.

Bei ya mafuta ya taa kwa bandari ya Dar es salaam imepungua kwa shilingi 49/lita ukilinganisha na bei zilizopita.

Taarifa hiyo imesema kuongezeka kwa bei kikomo kunasababishwa na mabadiliko ya bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB), gharama za uagizaji mafuta (premium) na kuongezeka kwa thamani ya dola ya Marekani ukilinganisha na shilingi.

Pamoja na mambo mengine taarifa hiyo ya Ewura haijaonesha kipengele cha ruzuku iliyokuwa inawekwa na Serikali kwenye kupunguza makali ya bei hizo.

Hatua hiyo inakuja ikiwa imepita miezi saba ambayo kwa muda wote serikali iliweka ruzuku hiyo baada ya bei za mafuta hayo kupaa katika soko la dunia.

Mei mwaka jana Serikali ilianza kuweka ruzuku ya Sh bilioni 100 kupunguza makali ya bei ya nishati hiyo.

Vivyo hivyo katika miezi iliyofuatia hadi Disemba mwaka jana iliendelea kuweka ruzuku hiyo kulinagana na mwenendo wa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Mathalani Julai na Agosti 2022, iliweka ruzuku ya Sh bilioni 100, Septemba ikashuka hadi Sh bilioni 65, Oktoba Sh  bilioni 59.58 wakati Novemba na Desemba hazikutajwa kiasi kilichowekwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

Habari Mchanganyiko

Bodi ya Maji Wami Ruvu kuchimba visima 10 kupunguza uhaba maji mikoa mitatu

Spread the love  BODI ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu imesema...

Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

Habari Mchanganyiko

NBC Dodoma International Marathon kutimua vumbi Julai 23

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetanganza msimu wa nne...

error: Content is protected !!