May 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bei mabasi ya mwendo kasi hadharani

Spread the love

BEI za nauli ya mabasi yaendayo haraka katika Jiji la Dar es Salaam zimetangazwa rasmi na kwamba viwango vipya vya juu vya nauli kuwa ni Sh. 400 kwa njia ya pembezoni, 650 njia kuu, na Sh. 800 kwa njia kuu pamoja na pembezoni, anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhi leseni kwa Kampuni ya UDA-RT leo Gilliard Ngewe Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) amesema upangaji wa nauli hizo umetokana na ukokotoaji wa gharama za uendeshaji uliofanywa na mamlaka hiyo.

“Desemba mwaka jana Kampnuni ya UDA-RT iliwasilisha kwa SUMATRA maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka, katika maombi hayo muombaji alianisha sababu za kuomba bei za viwango vya nauli,” amesema Ngewe.

Ameainisha sababu hizo ikiwa ni pamoja na ukubwa wa mtaji na gharama za uendeshaji, gharama za kulipia miundombinu, na matarajio ya ujazo wa mabasi kuwa chini kwa kuwa mabasi hayo yatakuwa yakitoa huduma kwa ratiba bila kujali ujazo wa abiria.

“UDA-RT awali walitoa maombi ya nauli kuwa Sh. 700 kwa njia za pembezoni, 1,200 kwa njia kuu, 1400 kwa njia kuu pamoja na pembezoni,” amesema.

Aidha, Ngewe amesema daladala ambazo zilikuwa zinafanya kazi katika barabara za DART zitakwenda kufanya kazi maeneo mengine na kwamba zitasaidia kuondoa adhabu ya usafiri.

Ronald Mwakatare, Mkurugenzi Mtendaji wa DART amesema kampuni yake imetenga siku mbili ambayo itaanzia kesho kwa lengo la kutoa elimu kwa abiria juu ya utumiaji wa mabasi hayo pamoja na mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji nauli.

Nauli hizo zitatozwa kulingana na ruti ambapo Mbezi mwisho hadi Kimara Sh. 400, Kimara hadi Kivukoni 650, Mbezi mwisho-kimara-kivukoni 800, Morocco-Kivukoni 650 na Kariakoo- Morocco 650.

error: Content is protected !!