September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bayern washeherekea ubingwa bila mashabiki

Spread the love

BAADA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Werder Bremen kwenye Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bundesliga, na Bayern Munich na kutangaza ubingwa wa Ligi hiyo, huku kukiwa hakuna mashabiki kutokna na zuio la serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Covid 19. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Bayern ambayo inachukua taji hilo katika misimu nane mfululizo toka mwaka 2003, baada ya kufikisha pointi 76, huku akiwa imesalia michezo miwili na kuonekana kutawala soka la Ujerumani kwa miaka ya hivi karibuni.

Bao pekee la Bayern kwenye mchezo huo lilifungwa na Robert Lewandowski ambaye mpaka sasa amefikisha jumla ya mabao 46, kwenye ligi hiyo na kumaliza pungufu kwenye mchezo huo baada ya mchezaji wao Alphonso Davies kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 79.

Licha ya kutwaa ubingwa mara zote lakini jana hali ilionekana tofauti hasa katika eneo la majukwaa kwa kutokuwa na mashabiki wao kama ilivyokuwa hapo zamani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa covid-19.

Baada ya kutangaza ubingwa jana, Bayern itakuwa imeweka rekodi ya kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo mara 30.

error: Content is protected !!