Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bawacha wamchongea kwa Rais Samia aliyewakataza kupanda miti Moshi
Habari za Siasa

Bawacha wamchongea kwa Rais Samia aliyewakataza kupanda miti Moshi

Grace Kihwelu
Spread the love

 

BARAZA la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Mkoa wa Kilimanjaro, wamemchongea kwa Rais Samia Suluhu Hassan mtumishi wa Shule ya Sekondari Kiboriloni, wilayani Moshi, aliyewakataza kupanda miti shuleni hapo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, yaliyofanyika leo tarehe 8 Machi 2023, mkoani Kilimanjaro, Mwenyekiti wa Bawacha Kilimanjaro, Grace Kihwelu, amesema kitendo hicho kilikuwa cha udhalilishaji lakini pia kiliwatia hasara baada ya kuondoka na miti yao waliyonunua kwa fedha zao.

“Mkoa wetu ni moja kati ya mikoa yenye joto kali sana, hata hapa naona mnavyoteseka. Sisi wanawake wa Chadema tuliamua kufanya zoezi la upandaji miti ya matunda na kivuli katika maeneo mbalimbali, tulifuata taratibu zote za maandalizi na kuanza zoezi hilo Ijumaa. Moshi tulikutana na ukinzani mkubwa mno katika Shule ya Sekondari Kiboriloni,” amesema Kihwelu.

Kihwelu amesema “Mheshimiwa Rais hakukuwa na sababu ya kupata taraifa hii lakini kwa kweli ubaguzi na unyanyasaji tuliofanyiwa Kiboriloni ulivuka mipaka kabisa, tulinyimwa kuotesha miti ile ambayo tuliinunua kwa pesa zetu. Moja kati ya mtumishi wa shule alifika akatukatalia akisema haturuhusiwi kuotesha miti pale maana sisi sio chama tawala, baada ya kupambana alisema analinda mkate wake tulilazimika kuondoka na miti yetu.”

Tukio la Bawacha kuzuiwa kupanda miti lilitokea tarehe 3 Machi 2023.

Katika hatua nyingine, Kihwelu amesema baraza hilo linampongeza Rais Samia kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kwa maridhiano waliyofanya ambayo yamebadilisha nchi.

“Maridhiano yamebadilisha nchi, kusitisha vilio vilivyotokana na ushindi katika uchaguzi, kunyimwa uhuru wa kukusanyika kutoa maoni na hofu. Hatua hii inawapa mhaho mkubwa wahafidhina kutoka serikalini na chama chako ambao walishazoea kunyanyasa,” amesema Kihwelu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!