July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bawacha bado si shwari, waliovuliwa uongozi, warejeshwa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Catherine Ruge, amevunja uongozi wa baraza hilo, kwenye majimbo ya Ilemela na Nyamaga, mkoani Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa za uhakika ambazo tumezipata zinasema, Ruge amechukua hatua hiyo, kama sehemu ya kulipiza kisasi, kufuatia baadhi ya viongozi hao, kutomuunga wakati wa uchaguzi wa kujaza nafasi ya katibu mkuu wa baraza hilo.

Katika uchaguzi huo, Ruge alikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wawili wa chama hicho, Ester Dafi na Asia Msangi. Tangu kumalizika uchaguzi huo, Ruge amekuwa akiwasaka wote waliokuwa wanampinga na kumtuhumu kutumia rushwa kusaka ushindi.

Kwa mujibu wa barua yake ya tarehe 4 Juni mwaka huu, Ruge anadai kuwa viongozi hao walifanya vurugu katika mkutano maalum wa baraza hilo, uliofanyika katika tarehe 3 Juni 2021, katika

Undani wa habari hii, kujua viongozi waliovuliwa na hatua ambazo, kaimu mwenyekiti wa Bawacha, Sharifa Suleman alivyoupinga uamuzi huo, soma gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumatano, tarehe 23 Juni 2021.

error: Content is protected !!