January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bavicha yaita vijana kugombea ubunge

Katibu Mkuu wa BAVICHA, Julius Mwita akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), juu ya vijana kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ngazi ya jimbo na kata.

Spread the love

BARAZA la Vijana Taifa wa Chadema (Bavicha), limewataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba mwaka huu. Anaandika Pendo Omary … (endelea)..

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita, amesema baraza hilo linawataka vijana kugombea uongozi ili waweze kuwa sehemu ya maamuzi katika taifa.

Amesema, kamati kuu ya chama katika kikao chake cha kawaida cha 22 Januari mwaka huu, ilipokea mapendekezo mbalimbali.

“Moja ya mapendekezo iliyopokea ni kuhakikisha Bavicha inakuwa na wabunge wa viti maalum ili kusimamia, kutekeleza na kufanikisha shughuli mbalimbali za baraza pamoja na kufanya uenezi wa baraza na chama kwa kuwa wabunge wa viti maalumu kikatiba wanakuwa na nafasi ya uenezi,” amesema.

Hatua hiyo inakuja baada ya kuzoeleka kuwa wabunge wa viti maalum hutokana na Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha)pekee.

Ameeleza kuwa, tarehe 6 hadi 7 Februari mwaka huu, kikao cha kamati ya utendaji ya Bawacha Taifa, kilikutana mjini Dodoma kwa mujibu wa muongozo wa baraza hilo kifungu cha 7.8.5 (h) ambacho kinaipa mamlaka ya kujadili na kupendekeza taratibu za kupata ubunge wa viti maalum kwa vigezo vilivyowekwa na kukubalika.

“Vigezo vya kuwapata wabunge ndani ya chama ni vya aina moja na kwa kuwa wabunge wote ni wa Chadema, sekretareti ya Bavicha taifa ilikubaliana na vigezo hivyo na kuamua kuvitumia kama vigezo ndani ya baraza la vijana lakini kwa nyongeza ya umri wa mgombea,” ameeleza Mwita.

Aidha baraza hilo, limeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuacha kufanya mzaha katika kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR).

“Kwa mkoa wa Dar es Salaam, NEC inafanya vichekesho. kwamba imetenga siku 12 tu za kuandikisha watu. Kama mkoa wa Njombe NEC ilitumia mwezi mmoja na zaidi, na wapiga kura wa Njombe wako laki 500,000, iweje Dar es Salaam yenye wapiga kura takribani 4 milioni uwatengee siku 12?,” Mwita amehoji.

error: Content is protected !!