August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bavicha wamnanga Rais Magufuli

Spread the love

BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) limemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli apunguze kutoa kauli zinazojenga chuki mioyoni mwa wa Tanzania, anaandika Jovina Patrick.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema,  Julius Mwita ambaye ni katibu mkuu wa Bavicha amsema kauli mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na Rais Magufuli ni hatari kwa umoja wa kitaifa.

“Rais Magufuli anapofurahia kupongezwa kwa mazuri pia akubali kukosolewa, kushauriwa na kupokea maoni, mawazo mbadala,” amesema.

Mwita amedai kuwa wananchi wanajenga chuki kutokana na kauli za Raisi na maelekezo yake, miongoni mwa kauli hizo ikiwemo kauli aliyoitoa kuhusu kuzuia mikutano ya hadhara ya vyanma vya siasa, huku wabunge na viongozi wa CCM wakitumia jukwaa la urais kufanyia mikutano yao.

“Je, CCM imekufa kiasi ambacho haiwezi kufanya mikutano yake yenyewe bila kutegemea mbeleko ya jukwaa la Urais?” Amehoji Mwita.

Aidha, Mwita ameshangazwa na kitendo cha Rais Magufuli kusema “wanasiasa wachunge midomo yao” wakati akijibu ushauri wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa, kuhusu kupelekwa mahakamni na kushtakiwa kwa masheikh wanaoshikiliwa mahabusu kwa muda mrefu sasa.

Amesema kuna ombwe kubwa la kiuongozi serikalini ambalo linasababisha wateule wa rais kulewa madaraka na kushiriki uvunjifu wa sheria kwa lengo la kumridhisha rais.

“Tunaunga mkono kauli iliyotolewa na Halima Mdee, mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema kuhusu wasichana wanaopata ujauzito kupewa fursa ya elimu baada ya kujifungua.

“Tunamwambia Rais Magufuli kuwa nchi inaendelea kuvimba na hatua za kuzuia kuvimba huku zisipochukuliwa, ni wazi hatutakuwa salama kabisa katika taifa hili,” amesisitiza.

error: Content is protected !!