August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bavicha waing’ang’ania UVCCM

Katibu Mkuu wa BAVICHA, Julius Mwita akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), juu ya vijana kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ngazi ya jimbo na kata.

Spread the love

LICHA ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) kusitisha mpango wa kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), limeshambulia umoja wa vijana wa chama hicho (UVCCM), anaandika Dany Tibason.

Manyanya Malambaya, Mwenyekiti wa Bavicha, Mkoa wa Dodoma amelitaka Jeshi la Polisi kumchukulia hatua kali Shaka Handu Shaka, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM kwa madai ya kuwaita wahuni.

“… lakini kauli ambazo zinaendelewa kutolewa na viongozi wa UVCCM kwa kuwaita wenzao wahuni ni kutaka kusababisha kuwepo kwa uvunjifu wa amani,” amesema.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo Manyanya pia amesema, kauli ya Shaka kwamba, wapo Dodoma kuikabili Bavicha ni ya kichochezi na kuamsha hasira za vijana.

Amehoji kuwa, UVCCM wana uhalali gani wa kuandaa vijana 3,000 kwa ajili ya kulinda mkutano wa CCM wakati Bavicha walisema wanataka kusaidiana na polisi kutekeleza kauli ya rais mwishowe wakiwekwa ndani?

“Kauli iliyotolewa na kiongozi wa UVCCM ni kauli ya kiuchochezi na tunalitaka Jeshi la Polisi kumchukulia hatua kiongozi huyo.

“Ifahamike, vijana wengi wa Bavicha ni waelewa na wametii kauli ya kiongozi wao mkuu (Freeman Mbowe) ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa.

“Haiwezekani viongozi UVCCM wakawa wanatukana na kujipatia uhalali wa kulinda mkutano wa CCM wakati tayari Jeshi la Polisi ndilo lenye majukumu ya kulinda mkutano kama walivyoeleza hapo hawali,” amesema.

Amesema kuwa, anataka ulimwengu ujue kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likilinda maslahi ya CCM na viongozi wake.

error: Content is protected !!