Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Basil Mramba afariki dunia
Habari MchanganyikoTangulizi

Basil Mramba afariki dunia

Basil Mramba
Spread the love

 

MWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Basil Pesambili Mramba (81) , amefariki dunia katika Hospitali ya Regency, jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya kifo hicho imetolewa na ndugu wa marehemu, Godfrey Mramba.

Godfrey amesema Mramba Mramba amefariki dunia leo Jumanne, tarehe 17 Agosti 2021, alipokuwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency.

Mramba amesema, amezaliwa tarehe 15 Mei, 1940, kuondoka tarehe 17 Agosti 2021.

“Kwa masikitiko familia ya Mramba inatangaza kifo cha baba yetu mpendwa, Basil Pesambili Mramba,” imeeleza taarifa ya Godfrey.

Godfrey amesema, kutokana na janga la Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19), familia itafanya mazishi binafsi.

“Kwa kuzingatia hali ya janga, familia inapokea sala zenu na tunaomba faragha. Tutapokea wageni kutoka kwenye familia pekee katika makazi yake yaliyopo Mawenzi Road Oysterbay,” amesema Godfrey.

Godfrey amesema msiba huo uko nyumbani kwa marehemu Mramba, Oysterbay jijini Dar es Salaam na kwamba ratiba ya mazishi itatolewa baadae.

Enzi za uhai wake, aliwahi kuwa Waziri wa Fedha (2001 hadi Desemba 2005). Waziri wa Viwanda na Biashara (2006 hadi 2008).

Pia, alikuwa Mbunge wa Rombo mkoani Kilimanjaro, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kutokana na utumishi wake, Mramba na Daniel Yona aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini mwaka 2016, walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwenda jela miaka mitatu kwa matumizi mabaya ya madaraka kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7

Hata hivyo, baada ya kutumikia adhabu hiyo kwa mwaka mmoja, walipunguziwa na kufungwa kifungo cha nje kuanzia Februari hadi tarehe 9 Novemba mwaka 2016, wakitakiwa kufanya kazi za jamii.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

error: Content is protected !!