Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Bashungwa atoa maagizo 10 kwa waajiri na waajiriwa wapya
Habari Mchanganyiko

Bashungwa atoa maagizo 10 kwa waajiri na waajiriwa wapya

Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa (Mb) ametoa maelekezo ya msingi mbalimbali yanayopaswa kuzingatiwa na waajiriwa na waajiri nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maelekezo hayo yamekuja baada ya kutangaza majina 16,676 ya watumishi wapya waliopangiwa vituo vya kazi katika Sekta ya Elimu na Afya nchini.

Orodha hiyo inatokana na waombaji wenye sifa waliokidhi vigezo baada ya Aprili, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan kutoa kibali cha ajira kwa kada za Ualimu na Afya, kwa ajili ya kuajiri walimu 9,800 wa shule za msingi na sekondari na wataalam wa afya 7,612.

Bashungwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 26 Juni, 2022 amesema waajiriwa wapya wote wahakikishe wanaripoti kwa wakurugenzi wa halmashauri walizopangiwa wakiwa na Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho ya NIDA, cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti halisi vyote vya Taaluma na Utaalamu wa Kazi vya mwajiriwa, ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira;

Pia waajiri wote wahakikishe wanapokea vyeti na kuviwasilisha baraza la mitihani kwa ajili ya uhakiki. Wizara ipewe taarifa mara moja kwa wale watakaokutwa na vyeti ambavyo ni vya kugushi ili hatua kali zichukuliwe;

Waajiri wote wahakikishe watumishi wapya waliopangwa kwenye halmashauri, wanapewa barua za ajira, na kuripoti kwenye vituo walivyopangiwa tu, na si vinginevyo;

Mwajiriwa mpya atakayechukua posho ya kujikimu, na baadaye asiripoti katika kituo chake cha kazi alichopangiwa, atachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria;

Waajiriwa wapya ambao hawataripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya siku 14, kuanzia tarehe ya tangazo hilo, watakuwa wamepoteza nafasi zao ambazo zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa, waliopo kwenye Kanzidata (Database) ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo Waajiriwa wapya wamepangwa, wahakikishe wanawapokea Waajiriwa wapya na kuwawezesha kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma, na baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao.

Taarifa za kuripoti waajiriwa hao zijazwe kwenye mfumo wa kielektroniki (ajira.tamisemi.go.tz), baada ya kila mtumishi kupokelewa na kukamilisha taratibu;

Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaelekezwa kukamilisha taratibu za ajira haraka, ili waajiriwa wapya waingizwe kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (HCMIS) mapema iwezekanavyo;

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wote wa Halmashauri, kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya OR-TAMISEMI yaliyotolewa kwenu Mwezi Machi, 2022, ya kuhakikisha mnafanya msawazo wa IKAMA ya walimu wa Shule za Msingi na Sekondari, ndani ya Mkoa na Halmasgauri kabla au ifikapo tarehe 30 Juni, 2022.

Ameagiza kutekeleza kwa bidii maelekezo hayo ili kuhakikisha shule zinakuwa na uwiano mzuri wa walimu, na taarifa

ya utekelezaji iwasilishwe kabla au ifikapo tarehe 15 Julai, 2022.

Amesema OR-TAMISEMI haitasita kumchukulia hatua Mwajiri ambaye hatatekeleza maelekezo haya ya kufanya msawazo wa walimu katika kuleta uwiano wa mwalimu, na wanafunzi wa 1:60 ulioelekezwa.

“Tunawaelekeza Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kushirikiana na Bodi zao za shule ili kufuata miongiozo ambayo Wizara imetoa kwa ajili ya michango ya wanafunzi wanaoendelea na masomo.

“Hatua kali zitachukuliwa kwa Mkuu wa Shule au Mwalimu Mkuu yeyote ambaye ataenda kuinyume na miongozo iliyotolewa na Serikali; na “Walimu waliopo kazini na Waajiriwa wapya, kuhakikisha wanafundisha wanafunzi kwa weledi, na bidii ya hali ya juu kwa kuzingatia kalenda ya ufundishaji iliyopo.

Wakuu wa Shule, Waratibu Elimu Kata, Maafisa Elimu wa Halmashauri na Mikoa yote nchini kufuatilia ufundishaji wa kila siku darasani, na kujiridhisha kuwa wanafunzi wanapata umahiri unaotarajiwa kwenye ngazi mbalimbali za elimu ya Msingi na Sekondari.

Aidha, amesema watumishi wote wa kada za Afya nchini, wanaoendelea na utumishi, na walioajiriwa wapya, kuhakikisha wanawahudumia wananchi kwa weledi na upendo wa hali ya juu, kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo ya utoaji bora wa huduma za afya nchini,”amefafanua Waziri Bashungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!