Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bashungwa amsimamisha kazi DED Mvomero kwa kupuuza maagizo yake
Habari za Siasa

Bashungwa amsimamisha kazi DED Mvomero kwa kupuuza maagizo yake

Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Hassan Njama ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili. Anaripoti Rhoda Kanuti Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 20, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Tamisemi, Waziri Bashungwa, amechukua hatua hiyo baada ya kushindwa kusimamia maagizo aliyompa tarehe 10 Machi 2022 alipofanya ziara kwenye Halmashauri hiyo.

Bashugwa amesema kuwa wakati alipokuwa akifanya ziara , alibaini upotevu mkubwa wa fedha za miradi na matumizi yasio sahihi ya kiasi cha shilingi 231.84 milioni, katika ujenzi wa shule ya sekondari Kumbukumbu ya Moringe Sokoine, fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula , jiko na bweni.

Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa

“Nilimuagiza mkurugenzi huyo kuwachukulia hatua za kiutumishi wakuu wote wa Idara na wahusika waliokiuka taratibu za manunuzi katika mradi huo.

“Hata hivyo hadi siku hii ya leo, hakuna Mkuu wa Idara yeyote au mtumishi aliyechukuliwa hatua kufuatia agizo lililotolewa,” amesema Bashungwa.

Aidha Waziri Bashungwa amesema anawataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini , kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu na kutoa taarifa mapema pale wanapobaini kuna ubadhilifu wa fedha za umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!