JORAN Bashange, Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha ACT-Wazalendo, amewataka wananchi wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam pamoja na Kata ya Mzimuni kumpigia kura Saed Kubenea Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia chama hicho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Bashange ameyasema hayo jana Jumapili tarehe 20 Septemba 2020, alipokuwa akifungua mkutano wa kampeni za mgombea udiwani Kata ya Mzimuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bakar Kasubi.
Bashange amesema, wanakinondoni haihitaji mbunge atakayekubali kununuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwamba kinamhitaji Kubenea aliyejitolea kupambana kwa ajili ya wananchi.
“Tunahitaji mbunge makini wa jimbo hili, hatuhitaji mbunge ambaye kuchaguliwa kwako sio kwa ajili ya biashara, kuchaguliwa kwake kuwe kwa ajili ya wananchi, mkienda kwenye kupiga kura mpigieni Kubenea na Kubenea Kinondoni itamelemeta,” amesema Bashange.

Amewaeleza wananchi wa Mzimuni kuwa Kubenea ni mwanasiasa mwaminifu mwenyekupenda haki na kwamba wananchi wanatakiwa kumchagua kwa ajili ya maendeleo yao.
Amesema kuwa wananchi hawapaswi kuirejesha madarakani Serikali ya CCM kwa kuwa imevunja Katiba kwa kuzuia mikutano ya kidemokrasia ilhali iliiapa kuilinda.
Katika Bunge la 11 lililomaliza muda wake, Kubenea alikuwa mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam kupitia Chadema.
Leave a comment