September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Basata lamfungia Nay wa Mitego

Spread the love

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana Emamnuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, msanii wa muziki wa kizazi kipya, anaandika Regina Mkonde.

Godfrey Mngereza, Katibu Mtendaji BASATA amesema, msanii huyo amefungiwa hadi hapo baraza hilo litakapojiridhisha kwamba, amtekeleza maagizo aliyopewa sambamba na kubadilika katika kubuni kazi zenye maadili na zisizo dhalilisha watu kutokana na kada zao.

“Maagizo aliyopewa msanii Nay ni adhabu ya kulipa faini ya shilingi milioni 1, kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa pale kati, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasimishaji sekta ya sanaa kwa maana ya kusajiliwa Basata,” amesema.

Pia amesema Nay anatakiwa kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kile alichokisema kwamba, anatoa kazi ya muziki yenye kuvunja maadili.

“Maamuzi haya yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23 ya mwaka 1984. Adhabu hizi zimetolewa kufuatia Basata kufanya kikao cha pamoja na msanii huyo jana siku ya Jumanne tarehe 26 Julai, 2016,” amesema.

Mngereza ametaja makosa ya Nay ambaye pia alikiri makosa hayo kwa maandishi ikiwemo la kujihusisha na shughuli za sanaa pasipo kusajiliwa na Basata pamoja na kutoa wimbo wa pale kati na kuuweka katika mitandao ya kijamii bila kuupelekea Basata ili kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.

error: Content is protected !!