July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Barwany ataka elimu ya gesi, mafuta

Mbunge wa Lindi Mjini (CUF), Salum Barwany

Spread the love

MBUNGE wa Lindi Mjini, Salum Barwany (CUF), ameitaka Serikali kutoa taaluma ya gesi na mafuta kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Katika swali lake bungeni leo, Barwany amesema kuna taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu juhudi za serikali za kutoa taaluma ya gesi na mafuta, na hivyo kuhoji wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wananufaikaje na ni vijana wangapi hadi sasa wamepatiwa mafunzo na wapi.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesema  tangu mwaka 2012/13, wizara yake imekuwa ikitoa ufadhili wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wa mikoa ya Lindi na Mtwara.

“Katika mwaka 2012/13, wizara ilifadhili wanafunzi 60 kutoka Mkoa wa Lindi na wanafunzi 50 kutoka Mtwara kusomea fani mbalimbali za ufundi katika Chuo cha VETA Mtwara.

“Aidha, mwaka wa fedha 2013/14, wizara imefadhili jumla ya wanafunzi 59 kutoka mikoa hiyo kusomea ufundi stadi,” alisema.

Amesema mpaka sasa, Shirika la Mafuta (TPDC), limechangia Sh. 10 milioni katika ujenzi wa maabara Mtwara na Sh. 15 milioni kwa ajili ya ujenzi wa maabara mkoani Lindi na Kisiwa cha Songosongo.

“Mwaka 2014, Kampuni ya Ophir Energy imejenga na kukarabati shule ya msingi Lilungu iliyopo Mtwara ambapo ujenzi umegharimu Sh. 600 milioni,”amesema.

Simachawene alisema pia, Kampuni ya utafutaji mafuta zinawekeza katika stadi zitakazohitajika kwenye sekta ya gesi asilia kwa kujikita katika kujenga uwezo wa wakufunzi, wanafunzi na wanunuzi wa vifaa katika kusadiai vyuo kutoa elimu kwa vitendo.

“Kwa mfano, Kampuni ya BG Tanzania inatekeleza mradi wa VETA awamu ya kwanza kuanzia Juni, 2012 mpaka 2015 kwa gharama ya Sh. bilioni 2.35,” amesema.

error: Content is protected !!