Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Barua ya Makanisa USA kwa Biden kuhusu Palestina Vs Israel
Kimataifa

Barua ya Makanisa USA kwa Biden kuhusu Palestina Vs Israel

Joe Biden, Rais Mteule wa Marekani
Spread the love

MAKANISA na Mashirika ya Kikristo nchini Marekani, yamemuandika barua ya pamoja rais mteule wa taifa hilo, Joe Biden kuhusu athari za uvamizi wa Israel nchini Palestina. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwenye barua hiyo, yamemtaka Bideni kuwalinda Wakiristo na Wapalestina wote kwa ujumla sambamba na kutekeleza sera mpya za kuunga mkono harakati za kuleta amani na haki.

Barua hiyo imeeleza kuwa, wanamtaka Biden kuangalia usalama wa Wakristo waliopo katika ardhi ya takatifu ya Palestina pamoja na wakazi wote ili waweze kuishi kwa amani na usalama.

Miaka minne ya utawala wa Donald Trump, Rais wa Marekani anayemaliza muda wake, imeshuhudia mabadiliko makubwa katika sera mbalimbali hususani Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na kutoa msaada mkubwa kwa nchi ya Israeli kuendelea kuwakandamiza Wapalestina.

Ili kufikia malengo ya amani, makanisa hayo yamesisitize azma ya Marekani ya kuunga mokono juhudi za kuleta amani ya haki na ya kudumu kutokana na mzozo kati ya Wapalestina na Waisraeli na kubadili sera ya nchi katika Mashariki ya Kati. Pia yamemsihi Biden kuhakikisha kuwa, pande zote mbili (Palestina na Israeli) zinaheshimiwa na kujumuishwa katika mazungumzo ya amani chini ya misingi ya sheria za kimataifa.

Benjamini Netanyau, Waziri Mkuu wa Israel

Makanisa yamemuomba Biden kurudisha uhusiano na Wapalestina ambao ni pamoja na kuruhusu kufunguliwa tena ofisi za uwakilishi wa Mamlaka ya Palestina mjini Washington ambazo zilifungwa na Trump. Pia makanisa hayo yameshauri Marekani kufungua tena ofisi za uwakilishi mjini Jerusalem na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kibalozi kwa Wapalestina bila kizuizi, kama ilivyokuwa hapo awali.

Wameelza kwamba, bila ushirikiano na Waplestina pia Waisraeli kwa pamoja, hakuna mabadiliko ya maana yanayoweza kutokea. Katika barua hiyo, makanisa hayo yamemtaka Biden kurudia msimamo wa Marekani kwamba, chini ya Sheria ya Kimataifa kuchukua hatua kuhakikisha Israeli inaadhibiwa kisiasa kwa ujenzi wowote wa makazi katika ardhi ya Wapalestina.

Mwaka 2019, utawala wa Trump ulitangaza kwamba Marekani haizingati tena makazi ya Israeli katika Mji wa West Bank kama kinyume cha sheria za Kimataifa. Kwa kuongezea, makanisa pia yamemuomba Biden kurudisha msaada na ufadhili kwa Mamlaka ya Palestina, Shirika la Usaidizi na Kazi la Umoja wa Mataifa (UNRWA) pamoja na taasisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa na za Haki za Binadamu zinazofanya kazi mjini West Bank na hata Gaza, hususani katika wakati huu mgumu ambapo ulimwengu unapambana na janga la ugonjwa wa corona (COVID-19).

Mahmoud Abbas, Rais wa Palestina

Barua hiyo ya kanisa imemuomba Biden kuhakikisha uwajibikaji kwa ukiukwaji wowote wa Haki za Binadamu unaofanywa na Israeli, na kuhakikisha kuwa ufadhili wa Marekani kwa Israeli hautumiwi kuendeleza kazi hiyo au kusaidia ukiukwaji wa Haki za Binadamu unaofanywa dhidi ya Wapalestina.

Israeli inapokea misaada mikubwa kutoka Marekani, ikipokea takriban Dola za Marekani bilioni 3.8 za msaada wa kijeshi kila mwaka.  Ufadhili huu huisaidia Serikali ya Israeli kudumisha uvamizi wa maeneo ya Wapalestina na kuifanya Marekani ijumuishe katika vitendo viovu vya Israel dhidi ya Palestina.

Biden pia ameombwa kurejea msimamo wa Marekani kwamba, maeneo yote yaliyochukuliwa na Israeli baada ya vita ya mwaka 1967 ikiwemo Jerusalem ya Mashariki na Golan Heights, hayatambuliki kama sehemu ya Israeli kama ilivyo chini ya sheria za kimataifa. Makanisa hayo na mashirika ya Kikristo yamemsisitiza Biden kutekeleza mchakato wa amani kwa uaminifu na uwazi kwa pande zote mbili (Palestina na Israeli) ili kuleta amani yenye haki na yakudumu.

Miongoni mwa Makanisa na Mashirika ya Kikristo yaliyotia sahihi katika barua hiyo ni Alliance of Baptists, American Friends Service Committee, Christian Church (Disciples of Christ), Christian Reformed Church in Northern America.

Office of Social Justice, Church of the Brethren, Office of Peace Building and Policy, Church World Service, Churches of Middle East Peace, The Episcopal Church, the Evangelical Lutheran Church in America.

The Friends Committee on National Legislation, Maryknoll Office for Global Concerns, Mennonite Central Committee US Washington Office, National Council of Churches of Christ in the USA, Presbyterian Church (USA), Reformed Church in America, United Church of Christ, and the United Methodist Church-General Board of Church and Society.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mpinzani mkuu wa Rais Kagame aachiwa huru

Spread the love  PAUL Rusesabagina, aliyewahi kuripotiwa kama ‘shujaa’ katika filamu ya...

Kimataifa

Rais Tshisekedi amteua kiongozi wa wanamgambo kuwa Waziri wa Ulinzi

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi,...

Kimataifa

Raila Odinga: Tutafanya maandamano makubwa mara mbili kwa wiki

Spread the love KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Raila Amollo Odinga ametangaza...

Kimataifa

Magharibi kuwekeza silaha Indo-Pacific, China yachochea

Spread the love KUVUNJIKA ushirhikiano wa China na Magharibi uliodumu kwa takribani...

error: Content is protected !!