Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Barua kuwang’oa kina Mdee yatua bungeni, Chadema yasema…
Habari za SiasaTangulizi

Barua kuwang’oa kina Mdee yatua bungeni, Chadema yasema…

Spread the love

 

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema kimesema, kimewasilisha barua kwa Spika wa Bunge kumweleza kuhusu hatima ya rufaa za waliokuwa wanachama wao, Halima Mdee na wenzake 18. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Ijumaa tarehe 13 Mei 2022 na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter.

“Barua kuhusu Baraza Kuu kutupilia mbali rufaa za waliokuwa wanachama 19 @ChademaTz imeshafika kwa Spika.”

“Hii ni barua ya pili baada ya ile ya kufukuzwa kwao uanachama na Kamati Kuu mwaka 2020. Spika ni vyema akaheshimu na kutekeleza sasa matakwa ya katiba ya nchi na sheria,” amesema Mnyika

Mdee na wenzake walifukuzwa Chadema tarehe 27 Novemba 2020 na kamati kuu ya chama hicho wakituhumiwa kughushi nyaraka za chama, usaliti na kisha kujipeleka bungeni jijini Dodoma kujiapisha kuwa wabunge wa viti maalum.

Baada ya kufukuzwa, walikata rufaa Baraza Kuu la chama hicho lililokutana juzi Jumatano tarehe 11 Mei 2022 na kumalizika jana pamoja na mambo mengine lilisikiliza rufaa zao na kuzitupilia mbali kwa kura 413 kati ya 423 zilizopigwa na wajumbe.

Tarehe 14 Februari 2022, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma alisema Mdee na wenzake wako bungeni kihalali.

Alisema hayo wakati akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari aliyetaka kujua uhalali ama uhalamu wa wao kuendelea kuwa bungeni licha ya kufukuzwa ndani ya chama chao.

Dk. Tulia aliyekuwa na siku chache tangu kuwa Spika akichukua nafasi ya Job Ndugai aliyejiuzulu tarehe 6 Januari 2022 alisema, Bunge halioni shida kuwaondoa wabunge na lilishawahi kufanya hivyo katika mabunge yaliyotangulia.

“Jambo linalosubiriwa ni kumaliza michakato yao ya ndani ya chama. Katiba yetu inasema mbunge lazima awe mwanachama, kwa hiyo wakimaliza wakaleta taarifa tutachukua hatua,” alisema Dk. Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini.

Mbali na Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha), wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Pia wamo, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara); Agnesta Lambat, aliyekuwa katibu mwenezi na Asia Mwadin Mohamed, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar na Katibu Mkuu, Bawacha-Bara, Jesca Kishoa.

Wengine ni, aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo.

Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

1 Comment

  • Duh!
    Mmetupilia mbali rufaa!
    Sasa ni nini hukumu yenu. Kwa nini Baraza Kuu lisiseme limeamua kuwafukuza pia. Waonekane wamefukuzwa mara mbili.
    Nyie ni chama cha siasa, msiendeshe maamuzi kama mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!