Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Barrick yaadhimisha Siku ya Wanawake kwa kutoa msaada hospitali ya Mwananyamala
Habari Mchanganyiko

Barrick yaadhimisha Siku ya Wanawake kwa kutoa msaada hospitali ya Mwananyamala

Spread the love

 

KATIKA kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Wafanyakazi Wanawake wa kampuni ya Barrick kutoka ofisi ya Dar es Salaam wametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kukabidhi vifaa mbalimbali vya kusaidia matibabu vilivyotolewana kampuni hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia wafanyakazi hao wamepata fursa ya kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo.

Akiongea na uongozi wa Hospitali hiyo leo Machi 7, 2023 Meneja Mawasiliano wa Barrick Nchini (Corporate Communications and Country Liasion Manager) Georgia Mutagahywa, amesema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu, pamoja na kampuni kuwa na programu mbalimbali za ndani pia imeandaa programu za kusaidia jamii.

Amesema Barrick, imekuwa ikitoa kipaumbele kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini ambapo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii imeweza kujenga vituo vya afya katika maeneo yanayozunguka migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara.

Kwa upande wake, Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo,Lilian Mwanga. ameishukuru Barrick kwa msaada huo sambamba na baadhi ya wafanyakazi wake kujitolea muda wao kutembelea hospitali na kutembelea wagonjwa walioalazwa hospitalini hapo ikiwemo Wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi..

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!