Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Barrick kulipa kiporo cha dola 300 mil
Habari za Siasa

Barrick kulipa kiporo cha dola 300 mil

Spread the love

RAIS John Magufuli amefanya mazungumzo na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold anayeshughulikia Afrika na Mashariki ya Kati, Dk. Willem Jacobs kuhusu utekelezwaji wa makubaliano yaliyofikiwa tarehe 19 Oktoba 2017 kati ya serikali na kampuni hiyo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa na serikali pamoja na Kampuni hiyo mwaka 2017, ni pamoja na Barrick Gold kuipa Tanzania dola za kimarekani 300 milioni kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato, na kulipa hisa ya asilimia 16 ya mgawo wa asilimia 50 ya mapato ya mauzo ya dhahabu kutoka katika migodi mitatu inayoimiliki.

Akizungumza katika kikao chake na Rais Magufuli kilichofanyika leo tarehe 20 Februari 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam, Dk. Jacobs amesema dhumuni la kikao hicho ni kumhakikishia Rais Magufuli kuwa makubaliano hayo watayatekeleza kikamilifu.

Dk. Jacobs amemhakikishia Rais Magufuli kwamba hakuna kitakachobadilika katika makubaliano yaliyofikiwa awali yaliyoongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Barrick Gold Corporation, Prof. John Thornton ambapo miongoni mwa makubaliano hayo ni kuilipa Tanzania kifuta machozi cha dola 300 milioni ambayo ni sawa na zaidi ya Sh. 682 bilioni.

Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema nyaraka za makubaliano hayo zimekamilika na kwamba kinachosubiriwa ni utekelezaji wa makubaliano hayo unaotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi mwaka huu.

“Baada ya muungano wao, hii sasa ni timu mpya na tumewaona ni watu ambao sasa wapo tayari kutekeleza yale yote yaliyokubaliwa, na sasa ni kwa kila upande kwenda kwenye vyombo vyake vinavyohusika kufanya maamuzi ya mwisho ili utekelezaji ufanyike,” amesema Prof. Kabudi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!