Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko North Mara yaeleza inavyodhibiti uchafuzi mazingira
Habari Mchanganyiko

North Mara yaeleza inavyodhibiti uchafuzi mazingira

Spread the love

 

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, umeeleza mikakati mbalimbali iliyofanyika katika kuhakikisha hausababishi uchafuzi wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji. Anaripoti Mwandishi Wetu Mara … (endelea)

Mgodi huo umeeleza hatua hizo baada ya kuwepo kwa tuhuma zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utiririshaji wa zebaki kwenye Mto Mara.

Meneja wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, amesema mbali na eneo husika kuwa umbali wa kilomita 80-85 chini ya mgodi, zebaki si sehemu ya orodha ya vitendanishi vinavyotumika katika mgodi huo.

“Kama kuna zebaki yoyote iliyopatikana katika mto haiwezi kuhusishwa na mgodi,” amesema.
Mbali na hilo, ameongeza kuwa Mamlaka ya Bonde la Maji ya Ziwa Victoria mara kwa mara imekuwa kichukua sampuli za maji katika maeneo yaliyo jirani na migodi.

Vilevile amesema mgodi wenyewe una mpango madhubuti wa ufuatiliaji wa maji ya ardhini na “hakuna ushahidi wa kuwepo zebaki au uchafu mwingine wowote kwenye maji ndani au karibu na maeneo ya uzalishaji.”
Aidha, alifafanua zaidi kuwa Serikali ya

Tanzania iliunda timu ya wataalamu inayoongozwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kwamba imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na mgodi huo ili kuhakikisha hakuna uchafuzi wa mazingira au maji unaotokea katika mgodi huo na katika maeneo yanayouzunguka.

Amesema mgodi huo umefikia lengo muhimu la uhifadhi wa taka zitokanazo na mchakato wa uchenjuaji wa madini kwa kupunguza kiasi cha maji yaliyohifadhiwa kutoka mita za ujazo milioni 7 hadi mita za ujazo 800,000 ndani ya kipindi cha miaka miwili.

“Kama ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Maelewano na NEMC. Haya ni mafanikio makubwa, ambayo yanaonyesha zaidi dhamira na jitihada za Mgodi wa Dhahabu wa North Mara zinakwenda sambamba kwa kuhakikisha hakuna uchafuzi wa maji au mazingira kwenye Mgodi na maeneo yanayouzunguka,” anasema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!