August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Barcelona wazuia wachezaji wake kwenye tuzo za FIFA

Tuzo ya FIFA

Spread the love

RAIS wa klabu ya Fc Barcelona Josep Maria Bartomeu ataongoza ujumbe wa klabu katika tafrija ya utoaji tuzo wa mchezaji bora wa FIFA, lakini wachezaji wa klabu hiyo waliopata mualiko kwenye sherehe hiyo hawataudhulia kutokana na timu kuwa katika maandalizi ya mchezo wake unaofuta siku ya Juma tano dhidi ya Athletic Club, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Barcelona watacheza mchezo wa marudiano katika dimba la Camp Nou baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Athletic Club ugenini.    

Mchezaji pekee wa Fc Barcelona alikuwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni Leonel Messi ambaye atachuana na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid wote kutoka ligi kuu nchini Hispania.

Tuzo hizo hapo awali zilikuwa zinajulikana kama Ballon d’Or lakini toka kuingia madarakani kwa rais mpya wa Shirikisho hilo la Soka duniani Gianni Infantino alibadilisha utalatibu huo na tuzo hiyo ya Ballon d’ Or iliendelea kuwa tuzo inayojitegemea kama ilivyokuwa hapo awali na FIFA kuwa na tuzo zaze ambzo zinatambilika kama The Best Fifa Awards.

Ujumbe wa klabu ya Fc Barcelona utaongozwa na Rais wa klabu hiyo  Josep Maria Bartomeu, makamu wa rais Jordi Mestre, mkurugenzi Silvio Elías, Mkurugenzi Mtendaji Oscar Grau, Albert Soler (mkurugenzi wa michezo mtaalamu), Robert Fernández  na Raúl Sanllehí.

error: Content is protected !!