December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Barcelona, Madrid, Liverpool waonja joto la jiwe

Spread the love

MICHEZO mbalimbali iliendelea jana barani Ulaya kwa kushuhudia magwiji wa tatau Liverpool, Barcelona na Real Madrid wakikubali kupokea vichapo ambavyo viliwashangaza wadau wengi wa soka kutokana na ubora wa vikosi walivyokuwa navyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Liverpool iliondoshwa nje ya mashindano ya Kombe la Ligi Kuu Uingereza baada ya kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Chelsea kwenye mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Anfield, huku mabao ya chelsea yalipachikwa na Emerson Palmeir 79 na Eden Hazard 85, bao la pekee la wenyeji lilifungwa na Daniel Sturridge katika dakika 58 ya mchezo.

Katika ligi kuu nchini Hispania Real Madrid walio kuwa ugenini kwenye uwanja wa Pizjuan walikubali kichapo cha bao 3-0 kutoka kwa Sevilla huku mabao hayo yakifungwa na Adre Silva katika dakika ya 17, 21 na Wissam Ben Yedder 39.

Huku kwa upande wa mahasimu wao Barcelona nao walipoteza mchezo kwa mabao 2-1 mbele ya Leganes kwenye dimba la Butarque, mabao ya wenyeji yalifungwa na Nabil Zhar 52, Oscar Arnaiz 53, kwa upande wa Barcelona lilifungwa na Philip Coutinho 12.

error: Content is protected !!