May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Barbara afunguka sakata la Morrison kuzuiliwa Afrika kusini

Spread the love

 

MTENDAJI mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez amekili kuwa, huwenda winga wao Bernad Morisson atakosekana kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini kutokana na kuwekewa kizuizi kuingia nchini humo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Simba itacheza na Orlando Pirates kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, mara baada ya jana tarehe 5 Aprili 2022, Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika “CAF” kuchezesha droo hiyo.

Akizumgumzia juu ya sakata hilo, kupitia kipindi cha michezo kinachorushwa hewani na kituo cha Wasafi, mtendaji huyo alikili kwamba klabu badio inafuatilia jambo hilo kama watafanikiwa kulitatua basi atakuwa sehe ya kikosi cha Simba kitakachosafiri.

Barbara Gonzalez, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba

“Kule nyuma alipata changamoto, anafamilia kule alipata changamoto na watu wa uhamiajia nab ado tunalifuatilia, kama akifanikiwa atakwenda na sisi, kikubwa bado tunafuatilia na lazima tufuate taratibu za nchi.” Alisema mtendaji huyo

Kwenye hatua hiyo ya robo fainali mchezo wa kwanza, Simba itakuwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam tarehe 17 Aprili 2022, huku mchezo wa marudiano utapigwa Soweto Afrika kusini Aprili 24 2022.

Mchezo huo utamkutanisha Morrison na waajiri wake wa zamani aliowatumikia katika kipindi cha miaka miwili kuanzia 2016 hadi 2018 na kisha kutimka na kujiunga na klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

error: Content is protected !!