September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Baraza la vyama ‘laikwepa’ Ukuta

Spread the love

SIKU tatu tangu Jaji Francis Mutungi, Msajili wa vyama vya siasa hapa nchini kutangaza kuwa, kikao cha Baraza la Vyama Vya Siasa kilichopangwa kufanyika siku mbili kabla Septemba Mosi mwaka huu, kitaamua hatima ya maandamano ya Chadema, mpango huo umeyeyuka, anaandika Pendo Omary.

Mkutano wa baraza hilo uliotarajiwa kufanyika tarehe 30 na 31 mwezi huu, huku Jaji Mutungi akidokeza kuwa, ungetoka na suluhisho la mvutano baina ya Chadema,Jeshi la Polisi na serikali juu ya marufuku ya mikutano ya hadhara sasa utafanyika 3 na 4 Septemba mwaka huu.

Vuai Ally Vuai, kaimu mwenyekiti wa baraza hilo, amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa, “Tumepitia orodha ya wahudhuriaji, tumegundua siku zilizobaki kufikia mkutano zisingetosha kwa wajumbe wemgi kuhudhuria.

Tumeamua kusogeza mbele mkutano huo hadi tarehe 3 na 4 Septemba, mwaka huu ili mkutano huo uwe wa ufanisi.”

Moja kati ya ajenda zinazotarajiwa kujadiliwa na baraza hilo ni pamoja na ajenda ya amani na utulivu wa nchi.

Mwanahalisi online ilitaka kujua, kwanini baraza hilo halijafanya juhudi za kuhakikisha wajumbe wa mkutano huo wanakuwepo katika tarehe zilizopangwa awali, ili suala la operesheni Ukuta ambayo imezua mabishano makali kati ya serikali na Chadema lipatiwe ufumbuzi.

Cons Akitandi, mwenyekiti wa fedha wa baraza hilo amejibu, “Ifahamike kuwa, hatukutani kwaajili ya Septemba Mosi, baraza lina vikao vya kila baada ya miezi mitatu na vikao vya dharula, haki haitapatikana katika mazingira ya shari.”

error: Content is protected !!