May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Baraza la usalama latoa taarifa kuhusu Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN)

Spread the love

BARAZA la usalama la Umoja wa Mataifa (UN), limetoa taarifa juu ya hali ya kisiasa nchini Burundi , ikiwa ni moja kati ya hatua zake za kulinda na kudumisha amani katika nchi za Africa, anaadika Catherine Kayombo.

Katika taarifa iliyosomwa na mwenyekiti wa baraza hilo, balozi Amr Abdellatif wa misri amebainisha kwamba hali ya kisiasa tete na hivyo kuongeza wakimbizi, mateso, mauaji ya kinyama na kutoweka kwa watu kadhaa.

Mwenyekiti huyo amesema baraza linasikitishwa na vitendo hivyo na kulaani vikali matamko katika umma.

Baraza hilo pia limekaribisha jitihada za nchi zinazoendelea ikiwamo kupokea wakimbizi kutoka Burundi.

Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadam na maelfu wengine kukimbilia nje ya nchi.

Mpaka sasa serikali ya Burundi haijaeleza lolote kuhusiana na ripoti ya baraza hilo.

error: Content is protected !!