May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baraza la NGO’s lapata viongozi wapya, wakabidhiwa majukumu

Spread the love

 

BARAZA la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO), limepata viongozi wapya kupitia uchaguzi wake uliofanyika jana tarehe 8 Julai 2021, jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Viongozi hao walitangazwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Uchaguzi wa NACONGO, Wakili Flaviana Charles.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo, Lilian Joseph Badi, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa NACONGO, wakati Revocatus Sono, akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, huku John Kiteve, akipata nafasi ya Mweka Hazina.

Wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo, ni wenyeviti wa kamati za NACONGO, ambao ni Novatus Marandu (Kamati ya Maadili). Gaidon Haule (Kamati ya Fedha na Utawala). Rhobi Samwelly (Maendeleo ya Uwezo) na Asifiwe Mallya (Utandaa na Mawasiliano).

Pia, katika uchaguzi huo walichaguiliwa wajumbe wa Bodi ya NACONGO, ambao ni, Jane Magigita, Revocatus Sono, Paulina Majogolo na Baltazar Komba.

Akizungumza baada ya kuwatangaza viongozi hao, Wakili Flaviana aliwataka wafanye kazi kwa weledi na kujitolea, huku akiwahimiza kutoa ushirikiano kwa Serikali, kwa ajili ya maslahi ya Watanzania.

“Nahimiza umoja na mshikamano katika kujenga NACONGO mpya, kwa manufaa ya sekta na Taifa kwa ujumla,”alisema Wakili Flaviana.

Aidha, mwenyekiti huyo wa uchaguzi, aliwataka wananchama wa baraza hilo kuvunja makundi yao ya uchaguzi, ili kuijenga NACONGO.

Huku akiwataka waliokosa nafasi kukubali matokeo na kusonga mbele, kwa kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ili kulijenga baraza hilo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa NGO’s, Richard Simbaiga, alisema uchaguzi huo umepita hivyo makundi yote yanatakiwa kuvunjwa.

Simbaiga aliwataka viongozi waliochaguliwa, kuwa wasimamizi wa asasi zote za kiraia bila ubaguzi, kwa kuzijali asasi kubwaa pekee yake.

Alisema takwimu zinaonyesha Tanzania kuna usajili wa NGOs zaidi ya 11,000, lakini zilizo kuwa hai hazizidi 4,000.

“Hivyo viongozi mnayo kazi ya kwenda kufanya, ambayo ni kuhakikisha hizi NGO’s zingine 7,000 ambazo hazijulikani zipo wapi, zinafufuliwa na kutoa machango katika kusukuma maendeleo ya taifa letu”alisema Simbaiga

Hata hivyo, aliwataka viongozi hao kuhakikisha kuwa wanaimarisha mifumo ya taasisi hizo, katika kufanya kazi zao kwa ufanisi.

error: Content is protected !!