March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Korosho yaondoka na mawaziri wawili

Spread the love

RAIS John Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya Baraza lake la Mawaziri ambapo Charles Mwijage na Dk. Charles Tizeba wametemwa. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Mwijage alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara huku Dk. Tizeba akiwa Waziri wa Kilimo.

Kwenye maadiliko hayo Mwita Waitara, Mbunge (mpya) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.

Mwita awali alikuwa Mbunge was Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam kupitia Chadema ambapo alijiuzulu na kurejea CCM kisha aliteuliwa kugombea ubunge kupitia chama hicho (CCM).

Taarifa iliyotumwa na Mkurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, imeeleza nafasi ya Dk. Tizeba imeshikwa na Japhet Hasunga, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Aidha katika nafasi ya viwanda na biashara iliyokuwa chini ya Mwijage, imechukuliwa na Joseph Kakunda, ambaye naye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa TAMISEMI.

Pia Rais Magufuli amemteua Constantine John Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, pamoja na kumteua Profesa Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora.

Aidha Rais Magufuli, amemteua Innocent Lugha kuwa naibu Waziri wa Kilimo, na uteuzi wa viongozi unaanza Novemba 10.

Pamoja na hivyo Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mama Anna Abdallah wa uenyekiti wa Bodi ya Korosho, pia ameivunja Bodi ya Korosho.

Walioteuliwa wataapishwa Jumatatu Ikulu Jijini Dar es salaam.

error: Content is protected !!