January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baraza la madiwani lamkataa mchumi

Jiji la Mwanza

Spread the love

ALPHONCE Mwakabesa-Mchumi wa Jiji la Mwanza, amekataliwa na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji kwa madai ya kutotimiza wajibu wake. Anaandika Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).


Hatua hiyo imefikiwa wakati baraza likijadili bajeti ya halmshauri hiyo kama kamati kabla ya kuipitisha kwenye kikao cha wazi.

Akizungumza juzi, Mwenyekiti wa baraza hilo, ambaye pia ni Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, amesema halmashauri haina sababu ya kuendelea na mchumi huyo kutokana na kushindwa kutambua utendaji wake wa kazi.

Amesema tangu kufika kwa mchumi huyo, maendeleo ya mipango ya halmashauri hiyo yameshindwa kusonga mbele kutokana na utendaji wake kutokidhi vigezo na kuomba mamlaka husika kumchukulia hatua.

“Hatuoni na wala haturidhiki na utendaji wake wa kazi kwani tangu afike hapa amekuwa ni mtu wa kuugua takribani miaka miwili, hivyo basi tunahitaji mchumi mpya ambaye atafanya jiji letu lizidi kusonga mbele,”amesema Mabula.

Mabula ameongeza kuwa, halmashauri hiyo inahitaji mtendaji aliye makini na ambaye ataipatia hadhi ya kuendelea kuwa jiji lenye mipango madhubuti kwa ajili ya manufaa ya wananchi.

Aidha, baraza hilo lilitoa siku 10 kwa mhandisi wa jiji, afisa afya, afisa utumishi pamoja na mwanasheria wa halmashauri hiyo kutoa taarifa za maendeleo katika kipindi cha mwaka 2012/13 kutokana na uzembe unaosababisha kutokamilika kwa miradi mbalimbali.

“Kuna miradi mingi kuanzia kipindi hicho na mpaka sasa haijakamilika kwa sababu ya uzembe wao, wakati fedha zilishatolewa, tunahitaji taarifa kamili ndani ya siku 10,”amesema Mabula.

Ameonya kuwa, kwa mtendaji yeyote asiyefanya kazi kwa ubora na ufanisi hana sababu ya kuendelea kuwepo katika halmashauri hiyo kwani ni mzigo unaosababisha hasara.

error: Content is protected !!