July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baraza la Famasia latuhumiwa kwa wizi

Spread the love

BARAZA la Famasia nchini limetuhumiwa vikali kuiba mali za Wamiliki wa Maduka ya Dawa Muhimu Dar es Salaam, anaandika Happyness Lidwino.

Hatua hiyo imeukera Umoja Wamiliki wa Maduka ya Dawa Muhimu Dar es Salaam (UWAMADAMUDA) ambao leo wamefanya maandamano hadi kwa Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni kufikisha malalamiko hayo. Hata hivyo, hawakumkuta.

Wakizungumza kwenye ofisi hiyo, wamiliki hao wamedai kuwa, baraza hilo limekuwa likipotosha ukweli kwa kutangaza kwenye vyombo vya habari kwamba, ndani ya maduka hayo kunauzwa dawa batili na kuwa, hawana vibali vya kuuza maduka hayo.

Akizungumza na mtandao huu, Juma Mganga, Mwenyekiti wa Uwamadamuda Taifa amesema, Baraza hilo lilisajili maduka yao na kuwatambua na baadae mwaka 2012 wamiliki wote walipelekwa kwenye mafunzo kwa lengo la kuwaelimisha namna ya kuboresha maduka hayo.

Amesema, mafunzo hayo yalitolewa na TFDA ambapo wamiliki zaidi ya 600 Dar es Salaam walishiriki na kila mmoja alilipa Sh. 300,000 zikiwa ni gharama za kuelimishwa namna ya kutoa dawa kwenye maduka.

“Baada ya kumaliza mafunzo, kila aliyehudhuria na kukidhi vigezo alipewa cheti cha kutambuliwa. Lakini cha ajabu ni kuwa, mara tu baada ya kumaliza mafunzo haya badala ya wamiliki hao kuendelea na kutoa huduma ya kuuza dawa za binadamu, walianza kufukuzwa mjini.

“Katika taarifa yao ambayo ilitolewa kupitia TFDA, waliainisha kuwa, wanatuondoa mjini ili watupeleke maeneo yasiyokuwa na maduka ya dawa, maeneo yaliyombali na sehemu muhimu za biashara, yasiyo na watu wengi na yenye hospitali za serikali zisizokuwa na dawa,” amesema Mganga.

Mwenyekiti huyo amesema, kwa uchunguzi waliofanya wamegundua kuwa, baadhi ya watumishi wa Famasia wanamiliki maduka ya dawa na famasi kuwa wapinzani wakubwa katika biashara.

“Pamoja na mafunzo yote walivyopewa na kuwa na vibali vya umiliki bado Baraza la Famasia limegoma kutupa vibali ambavyo tuliahidiwa kupewa baada ya kumaliza mafunzo ili tuanze kulipa kodi, kitendo cha kutufungia na kutufukuza kinaikosesha serikali mapato,” amesema mmoja kati ya wamiliki hao.

“Baraza la Famasia lina ajenda iliyojificha ambayo kiujmla ni kutaka kuliteka soko la dawa, ndio maana hata wakichukua dawa zetu hawatangazi ni za kiasi gani? Wala hazifikishwi sehemu husika,” wameeleza.

error: Content is protected !!