April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Barakoa zawa ‘deal’ jiji la Dodoma

Spread the love

KUTOKANA na kuwepo kwa mahitaji ya matumizi ya barakoa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kifaa hicho kimekuwa lulu katika jiji la Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). 

Hali hiyo imetokana na serikali kutoa maelekezo ya kuvaa barakoa kwa ajili ya kujilinda na virusi hivyo na wananchi kuwa na mwamko wa kuelewa na kujali matumizi ya barakoa.

Hali hiyo imeonekana baada ya uchunguzi na utafiti wa gazeti hili na kubaini kuwa barakoa kuwa hadimu katika maduka mengi ambayo yanauza madawa ya binadamu pamoja na vifaa tiba.

Kitendo cha barakoa kuwa adimu katika maduka halali ya kuuza madawa baridi ya binadamu imepelekea mafundi chelehani kuanza kufanya biashara ya kushona barakoa na kuanza kuzitembea mitaani.

Katika kuthibitisha kuwepo kwa uhaba wa barakoa madukani, Meneja wa duka la Nakiete Jijini Dodoma, Attilio Elia, alisema suala la barakoa limekuwa changamoto kubwa katika upatikanaji wake hasa tangu serikali kutoa maelekezo ya kuwepo kwa matumizi ya barakoa.

Alisema kuwa baada ya serikali kutilia mkazo wa utumiaji wa barakoa, Nakiete imekuwa msitari wa mbele katika kutafuta barakoa ambazo zipo katika viwango ambavyo vinatakiwa kwa mujibu wa sheria ya viwango kwa ajili ya kuwapatia wateja wao.

Hata hivyo alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya upatikanaji kutokana na jamii kuwa na mwamko mkubwa wa kutumia barakoa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Hata hivyo meneja huyo alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa tatizo kubwa lakini Nakiete imekuwa ikijitahidi kuhakikisha inatafuta barakoa ambazo wanawauzia wananchi kwa bei ambayo inatakiwa na siyo bei ya kurusha.

Kuhusu utumiaji wa vitakasa mikono alisema kuwa Nakiete tawi la Dodoma limekuwa likishirikiana na wadau mbalimbali kutoka vyuo vikuu kwa lengo la kupata bidhaa ambazo ni bora na zinazoweza kukidhi viwango kwa faida ya watumiaji.

Kuhusu upandishwaji wa bei kwa baadhi ya watu ambao siyo waaminifu alisema kuwa kuna kila sababu ya kutopandisha bei ya vifaa hivyo kwani iwapo vitapandishwa kiholela itasababisha ugonjwa kuenea zaidi.

Sophia Mohamed mkazi wa jiji la Dodoma, alisema kuwa wapo ambao wanavaa barakoa kama sehemu ya ujiko au ubishoo bila kuzingatia muda halisi wa matumizi ya barakoa.

Pia alitiilia shaka matumizi ya barakoa ambazo zinatengenezwa mitaani  na kueleza kuwa kuna uwezekano wa kutafuta ugonjwa mwingine ambao unaweza kuwa hatari zaidi ya Corona.

error: Content is protected !!