May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Barakoa zatawala mkutano Rais Samia, wazee Dar

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekwisha kuwasili ukumbi wa Mliman City, Dar es Salaam, ambapo atazungumza na wazee wa mkoa huo. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Mkutano huo na wazee, unafanyika leo Ijumaa, tarehe 7 Mei 2021.

Zaidi ya wazee 900 wamejitokeza kwenye ukumbi huo pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Viongozi wote akiwemo Rais Samia, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wazee, wamechukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19), kwa kuvaa barakoa.

Hii ni mara ya kwanza kwa shughuli kubwa kama hiyo kufanyika na kushuhudia wakiwa wamevalia barakoa.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

error: Content is protected !!